The Eternal Christ

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 5 views
Notes
Transcript

John 1:30

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika mlango wa kwanza vs.30. Wiki iliopita tuliona Yesu kufika, huyu mtu Mtume Yohana, mwandishi ya kitabu hiki na Yohana Mbatizaji wanaongea kuhusu. Ikiwa ni mara ya kwanza sisi tumesoma bibilia na tumeanza na kitabu cha Yohana tungesoma soma hizi mistari yote 1-28 na tungeshangaa kusoma kuhusu huyu mtyu ambaye ni kila kitu, ni Mungu, Vyote viliumbwa ndani yake, yeye alikuwa nuru ya watu alikuwa uzima, ikiwa ni mara ya kwanza tulisoma hii tungetaka sana kujua huyu mtu ni nani na tulisoma vs.29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake. Tumeambiwa huyu mtu ni Yesu.
Yesu. Yesu, kuzaliwa kwake kulitabiriwa na Isaya miaka mia saba kabla ya hii yote, Isaya 7:14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli. tunasoma unabii huu ulitimia kwa kitabu cha Mathayo 1:22-23 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. Hizi mistari zinaanza na hayo yote yamekuwa, ni nini? Ni Malaika wa Bwana alikuja na aliongea na Yusufu na alimwambia na alisema Mariamu anabeba mtoto wa Roho Mtakatifu na tunasoma vs.21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Tunasoma anaitwa Yesu. Baba yake kwa hii dunia alikuwa Yusufu alikuwa seremala, mama yake alikuwa Mariamu, binamu wa kwanza au first cousin yake alikuwa Yohana Mbatizaji. Huyu Yesu ambaye alikuwa na ndugu lakini kusema ukweli walikuwa half brothers kwa sababu walikuwa na baba tofauti. Baba Wa Yesu alikuwa Mungu.
Tumeshaa ona Kwa Yohana 1:14 kama Yesu pia alikuwa Mungu na sasa alizaliwa na aliwekwa mwili kama sisi. Huyu Yesu ambaye aliumba kila kitu, alikuwa Mwana kondoo wa Mungu, atakuwa dhabihu ya dhambi kwa ulimwengu wote sasa anasimama mbele ya Yohana Mbatizaji.
Tusome mistari yetu ya leo. Yohana 1:30-34 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji.Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu. hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Vs.31 tunaona Yohana Mbatizaji kutangaza kwa kila mtu, mbele ya Yesu bila shaka ya kwamba Huyu, Yesu ni ule mtu ambaye alikuwa nyuma yake lakini alikuwa mbele ya yake. Watu wote ambao wanabatizwa na Yohana sasa macho yao wamewekwa kwa yesu. Na kama Yohana anasema hapa anasema huyu ni Mungu, Alisema alikuwa kabla yangu. Sisi tunajua Yohana Mbatizaji alizaliwa miezi sita kabala ya Yesu. Wakati Yohana anasema hii kwa watu ni kusema huyu Yesu alikuwa, Ni yule Wayahudi wangejua jina lake, MIMI NIKO AMBAYE NIKO, I AM. Ni Yeye katika utimilifu wake sisi tulipokea neema juu ya neema, Ni Yeye Yohana anasema mimi si stahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake. Tena hapa Yohana Mbatizaji anajiweka chini na anainua Yesu. Hii ni mfano mzuri kwa viongozi wote wa kanisa. ni mzuri kufahamu kanisa si biashara, kanisa si kuhusu kiongozi fulani, kanisa si kuhusu mamlaka au pesa au kitu cho chote kiingine. Kanisa ni kumhusu Yesu kwa sababu ni yake. Niliona Pastor moja alipost kitu kusema, “Kanisa si ya mtu moja ni ya sisi wakristo” Pole sana lakini kanisa ni ya mtu moja, ni ya yesu kristo, si yetu wakristo, sisi ni wake. Imagine ikiwa sisi sote, viongozi na wakristo tunaweza kufanya kama Yohana Mbatizajina kujiweka chini na kuweka macho ya watu wote kwa Yesu. Kanisa litabarikiwa sana. Siku hizi ni kama mapastors wanajaribu kuweka macho ya watu wao kwa kila kitu, hata hawataki watu kuona Yesu, wanataka watu kuona pastor yao ni mtu wa nguvu, pastor yao ako na mamlaka, na unaweza kujua hiin i ukweli wakati Bibilia, neno la Mungu inabaki bila kufunguliwa, Mapastors siku hizi hawawezi kujitayarisha kuhubiri mahubiri kutoka neno la Mungu, wengi hawajui kufanya hii na wengine wakifanya hii itaweka macho ya watu kw mungu wao na si kwa pastor mwenyewe. Chunga sana! kwa nini wanafanya hii? Yesu alisema wazi sababu wanafanya hii. Angalia Mathayo 23:4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. Wanaweka sheria mingi sana juu ya watu wao lakini hata hawa wenyewe hawawezi kufanya. Mara ya mwisho Pastor aliweka pesa kwa sadaka ni lini? Mara ya mwisho yeye alitoa mbuzi moja kusadia mtu ambaye ako na shida kanisani lake ni lini? Mathayo 23:5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; Kila kitu wanafanya ni mbele ya watu kuona lakini badaye Yesu anasema ndani ya hawa wamejaa unang’anyi na kutokuwa na kiasi. Ni wanafiki! Hupanua hiziri zao huongeza matamvua yao. Wanavaa suiti smart sana, kalamu ya dhahabu, viatu vinag’aa. Ni kusema nje hawa ni mara dari sana lakini wanavaa vitu hivi kujaribu kuficha unafiki wao.
Mathayo 23:6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, Kwa sherehe wanataka watu kuona hawa ni wakubwa, hawa ni watu muhimu na wanaketi Mbele, hata labda imeandikwa VIP, Mtu wa muhimu na watu wa kawaida hawawezi kuketi hapo. Ni kusema angalia mimi, mimi ni kitu. Hata kwa masinagogi, kanisa, utapata hawa kwa kiti cha muhimu sana, kiti kubwa kwake na labda bibi yake, Mama kanisa. Kama mfalme wana viti vyao.
Mathayo 23:7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. Kila mahali wanaenda wanapenda sana kuitwa Pastor. kwa sababi hii jina iko na mamlaka, Wewe ni Man of God!!! Watu watataka kusikia kama unasema, wewe ni Mungu ni karibu sana. Wale wamejiweka kwa nafasi ya Bwana wao Yesu kristo. Na hapa tuko na Yohana Mbatizaji, Yesu alsiema Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; Na tunaona kama anafanya. Anajiweka chini na anaweka macho ya watu kwa Yesu.
Rudi kwa Yohana 1:31.Wala mimi sikumjua. Sisi tunajua Yohana Mbatizaji na Yesu walikuwa Cousins, si kama Yohana hajamjua Yesu lakini hii ni kumaanisha hajamjua kama alikuwa Masihi. Pia inamaanisha Yesu na Yohana hawajakuwa na mkutani kabka ya hii siku kupanga kudanganya watu kama walimu wa uongo leo na wanaoanga watu kufika mbele kwa stage na wanaponyesha hawa na hata hawajakuwa na shida. Yohana anasema hapa, haijakuwa naam na hiyo. Anaendelea kusema vs.31 lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. tena Yohana Mbatizaji alisema hapa, hajafika kuanzisha ministry yake hajafika kujenga jina lake lakini alikuja kubatiza watu kuonyesha hawa walihitaji kutubu kwa dhambi zao na kujitayarisha kwa Masihi wao, huyu Yesu amekuja na yeye ni Masihi na ameleta ukombozi kwao. Kila kitu Yohana amehubiri, hii manneo yote ya kubatiza watu sasa sababu amefanya hii yote inasimama mbele ya wote, ni Yesu.
Kumbuka Lengo ya kitabu hiki ni kuonyesha wasomaji ya kwamba Yesu ndiye Kristo. Tunaona tena kitu cha ajabu inafanyika hapa kwa Vs.32-33 Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Sasa hapa Yohana Mbatizaji anasema Mungu alimwambia vitu hivi, hakuna mwengine anaweza kusema kitu kama hii. hatujui jinsi alivyofunua hili kwa Yohana, lakini alifanya hivyo. Vs.33 Yohana aliambiwa, Mungu alimwambia ni mtu utaona wakati utambatiza, ni kitu cha ajabu kitafanyika, Utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake.
Tunaona hii wakatu Yohana alibatiza Yesu. Tunaona hii katika kila injili, Mathayo< marko Luka na Yohana. Ni mzuri tuangalia yote. Mathayo 3:16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; Marko 1:10-11 Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe. Luka 3:22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe. Yohana Mbatizaji alikuwa hapo, ni yeye anabatiza Yesu, hajataka kubatiza Yesu, sasa fikiria Mungu wa kila kitu anasimama mbele yako na anataka kubatiza, utajibu nini? Tunaona kama Yohana Mbatizaji alijibu kwa kitabu cha Mathayo 3:13-15 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Yohana Mbatizaji kusema ukweli hakuna msahidi mzuri zaidi ya yeye kwa sababu ni yeye alikuwa hapo, ni yeye alisikia hii sauti ya Mungu kusema vitu hivi.
Rudi Kwa Yohana 1:32 Tena Yohana akashuhudia akisema, Nataka hapa sisi kuona kitu. Jina lako ni muhimu sana. Kusema ukweli huna kitu cho chote bila jina lako. Ukiharibu jina lako, ni ngumu kupata kazi, hata loan ya banki, ni ngumu sana kukuamini. Unaweza kutumia miaka mingi sana kujenga jina lako na dakika moja ukifanya kitu kibaya umeharibu jina lako. Tuko mahali mingi bibliani inatuambia kuhusu hii, lakini mahali moja na ni mzuri tushike kama inasema ni Mithali 22:1 Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; ni ajabu sana. Jina lako ni muhimu.Zaidi ya mali nyingi. Unaweza kuwa na kitu cho chote ikiwa uko na mali nyingi, lakini bado jina jema ni mzuri zaidi. Ikiwa wewe ni mkora, huwezi kuwa na jina jema, ikiwa wewe ni mlevi huwezi kuwa na jina jema, mwizi, mwongo hii yote, chunga sana jina lako. Yesu alisema kwa kitabu cha Mathayo 5:37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu. Anasema usicheze na maneno yako, kwa sababu utaharibu jina lako, watu watakujua kama mtu ambaye si mwaminifu. Ukisema Ndiyo, ni nidyo na watu wanajua ni ukweli, ukisema hapana, ni hapana na watu wanajua ni naam na hiyo. Ikiwa mtu anasema, ukokaribu kufika Narok na unasema, Ndiyo nikokaribu na umetoka sekenani saa hii, hii ni uongo. Sema ukweli haafu wakati wewe unatoa ushuhuda kuhusu kitum watu wataamini. Shida ya mapastor wingi sana siku hizi ni hawa ni wakora zaidi, ndiyo si ndiyo kwao na wakati wanajaribu kuongea kuhusu Yesu watu hawaamini hawa. Kitu cha kwanza watu wanajaribu kuharibu wakati wako na shida na wewe ni jina lako, kwa sababu ikiwa jina lako ni mbaya, ushuhuda wako haibebi uzito.
Sasa hapa tuko na Yohana Mbatizaji, hakuna mtu mzuri kama yeye wamezaliwa na anatoa ushuhuda kuhusu kitu na ni lazima tunasikia. Anasema kwa vs.32 Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Nimesimama kwa maji na huyu anaitwa Yesu, Nilimbatiza na nimeona kama nimeambiwa na Mungu nitaona juu ya Masihi, niliona Roho kama Hua kuja kutoka mbinguni na akakaa juu yake. Hii ilikuwa Roho Mtakatifu Yohana aliona na alisema ilikuwa kama Hua, Dove, Hii ndege ni ishara hata siku zetu ya Upendo na huzuni, na tunaona akakaa juu yake. Hajafika na alirudi alikaa na Yesu.
Baada ya hii yote tunasoma maneno ya Yohana Mbatizaji kusema kwa vs.34 Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu. Sasa hii ni mwisho ya ushuhuda wa Yohana Mbatizaji kumhusu Yesu. Tukiangalia vizuri tutaona Yohana Mbatizaji alikuwa na mambo saba aliyoshuhudia kuhusu Yesu. Ya kwanza alishuhudia uwepo wa yesu. Tulisoma Yohana kusema amekuwa mbele yangu. Ni kusema ni Mungu, hana mwanzo na hana mwisho. Kitu cha pili alishuhudia Ubwana wa yesu. Alisema yeye ni sauti ya kusema inyosheni njia ya bwana. Kitu cha tatu alishuhudia ubora wake usiopimika, alisema Yesu ni Mkuu kabisa, kumbuka alisema hata sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake. kitu cha nne alishuhudia kazi ya dhabihu. Tazama! Mwana kondoo wa Mungu! Kitu cha tano alishuhudia ukamilifu wake wa kimaadili. Wakati tulisoma ya Yohana Mbatizaji aliona dua kufika na kukaa juu ya yesu. kitu cha sita alishuhudia haki ya Yesu kubatiza kwa Roho Mtakatifu na kitu cha saba alishuhudia uwana wake matakatifu. kama amesea hapa kwa mstari ya mwisho yetu, huyu ni Mwana wa Mungu. Hii yote tunaweza kusema yOhana Mbatizaji anasema ni hii, Masihi amefika, Ni mzuri kumtambua yeye ni nani, Yeye ni Mwana wa Mungu, Mwana Kondoo wa Mungu dhabihu ya mwisho kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu.
Natumiani sana umeona Yesu ni nani. Utakuwa ushuhuda gani wa maisha yako kuhusu Yesu ni nani? Ikiwa hujatubu kwa dhambi zako na ikiwa hujaamini katika Yesu kristo, yeye ni kitu cha hofu kwako na ni mzuri kwa sababu hukumu inakuja, lakini kwetu ambao tumeamini, tumetubu, tumesemehewa kwa dhambi zetu, yesu ni tamu sana, Yesu tumaini letu, faraja yetu, yeye ni kila kitu kwetu. Hata leo asabuhi anaweza kuwa hii kwako. Ni kutubu na kuamini. Ukitaka kuongea zaidi au uko na maswali, tafadhali baada ya ibada yetu kuja hapa mbele kuongea na mimi au unaweza kukaa tu kwa kitu chako na nitakuja kwako. Lakini tafadhali usitoke hapa leo asabuhi bila kufikiria vitu hivi.
Asanteni sana, bwana wetu yesu kristo asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.