How to know?

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 10 views
Notes
Transcript

2 Corinthians 5:17

Leo asabuhi nilitaka kutoka kitabu cha Yohana na kuongea kuhusu kitu ambacho ni muhimu sana na nimefikiri kwa sababu tuko karibu kuingia mwaka mpya itakuwa mzuri kwetu kufikiria vitu hivi. Lakini ninaulizwa swali mingi na watu lakini swali la kwanza ni hii, Ninweza kujua bila shaka ikiwa nimeokoka? Hii ni swali nzuri sana, kwa sababu milele ni ukweli, baada ya sisi tunatoka hii dunia, tunakufa tunaingia milele, na tutaingia mbinguni pamoja na Yesu au tutaingia jehanmu, Mahali ambapo tutatengwa na Mungu. wakati mtu anauliza ikiwa anaweza kujua ikiwa ameokoka karibu kila wakati anauliza ikiwa atenda jehanamu wakati anakufa, hii ni hofu watu wengi wako nai maishani yao, labda hata wewe uko na hii hofu. Lakini ni mzuri kujua ya kwamba wakati unauliza ikiwa unaweza kujua ikiwa umeokoka ukweli ni kujua ikiwa dhambi bado inatawala maishani mwako. Na ukipata jibu la hii, utajua ukweli. Ikiwa dhambi ni Bwana wako halafu bado wewe hujaokoka, Ikiwa Yesu ni Bwana wa maisha yako na unapigana na dhambi kila siku, kila dakika, halafu utajua wewe ni Mkristo na umeingia hii vita ya maisha ya Mkristo.
Kumbuka wakati tulisoma kitabu cha Wagalatia na tulifika 5:16-17 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Hii ni mtu ambaye ameingia vitani. Hii mtu ambaye ameokoka kweli kweli. Nitauuliza ikiwa wewe ukovitani au wewe ukosawa kabisa na unaishi maisha yako kama unataka. Unajaza maisha yako na vitu ambavyo viankupendeza, tamaa zako au unafuata yesu kristo na unapigana na hii mwili na tamaa zake?
Kwa hii mwaka mpya nilitaka kutupea mtihani, nataka sisi sote kufanya na kuona ikiwa tunajua Yesu ukweli, ninataka sisi kujua bila shaka tuko kwa njia gani ya Yesu aliongea kuhusu kwa kitabu cha Mathayo 7:13-14 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. Wewe uko kwa njia gani? Si ngumu kujua. Lakini matokeo ya njia unaenda saa hii, ni ya milele.
Youth, Wazee sisi sote tunadhani tuna wakati, hii dunia imetudanganya kutuambia kujaza maisha yako na kila kitu unataka na iko sawa, dunia inawaambia Youth ukiwa mdogo, furahia mwenyewe, kwa sababu siku moja utakuwa mzee. Hakuna mtu ako na ahadi ya kesho, watoto wadogo na Youth wanakufa kila siku. Ukisearch utaona kila siku Youth kati ya umri kumi na tatu na ishirini 4,500 wanakufa kila siku. Watoto miaka tano na chini karibu 14,000 wanakufa kila siku kwa hii dunia. Kusema ukweli time ni kitu ambacho hakuna mtu ako nai. Leo nataka sisi kujua bila shaka tumeokoka au hatujaokoka.
Tusome mstari yetu ya leo Waraka wa pili wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Sasa msatri yetu ya leo inaanza na hata imekuwa. Hii hata imekuwa ni muhimu sana, kumbuka muktadha ni kila kitu wakati tunasoma bibilia. Hii yote inaanza kwa vs.1 na Paulo anaongea kuhusu vitu ambavyo ni ya muda na ya milele na anaongea kuhusu maisha haya. Anasema hata ikiwa tunapoetza maisha yetu tuko na maisha ingine na ni Mungu ametengeneza hii maisha ingine ambaye inatuongojea. Kusema ukweli Hapa kwa hizi mistari Paulo anatuonyesha mtu ambaye ni mkristo kweli kweli na anaweza kujua naam na gani, bila shaka. Wakati tunasoma vitu hivi ya hizi mistari nitasema kujipima na vitu hivi kuona ikiwa ni tamaa ya moyo wako na kama unafikiri kuhusu vitu kama maisha haya. Vs.4 anasema Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima. Wakati tuko hapa kwa maisha haya ni ngumu sana kwa sababu tumebadilishwa ndani tuko na Roho mpya anaishi ndani yetu na tunataka kuwa pamoja na Bwana wetu. Hii ni kila kitu kwetu na hata tunaweka macho yetu na mawazo yetu kwa siku ile wakati tutakuwa pamoja naye. lakini saa hii tuko hapa. Vs.6 Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. Kwa sababu ya hii anasema vs.7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.) Kwa maisha haya sisi ni watu wa imani, hatuwezi kuona vitu hivi lakini tunaamini sana, tunajua ni kazi Mungu amefanya maishani yetu na tunaamini. Hii dunia na kila koitu ndani yake haiwezi kutuambia tofauti. Sisi ni mbegu nzuri ilyopandwa katika udongo mzuri. mizizi yetu iko kwenye kina kirefu. Sisis si mbegu iliyoanguka juu ya mwamba na isiyo na mizizi, na jua linachomoza na kutuchoma , na wasi wasi wa ulimwengu hupata furaha yetu. Hii si mtu ambaye anajua bila shaka, kwa sababu twaenenda kwa imani.
Vs.8 Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. Tunatamani sana kuwa pamoja na Mungu wetu. Hii ni mtihani mzuri sana. Watu wengi wanapenda hii dunia na vitu ndani yake, wanapedna hata zaidi ya kufikiria siku ile watakufa. Ikiwa wewe ni mtu ambaye hunatumaini, imani yako si kwa yesu kristo, unaona kifo kama ni kitu kibaya sana, hujashika ya kifo inakupeleka kuwa pamoja na bwana wako, kifo ni mwanzo ya milele. Tamaa yetu ya wakristo ingekuwa kuwa pamoja na bwana wetu na tungetamani sana siku ile. Hakuna mtu anataka kufa lakini ni kusema sisi wakristo wa kweli hatuna shaka yo yote, siku ile tunajua inakuja na ni furaha kwetu kuwa pamoja na Yesu. Ni huzuini kwetu wengine kwa sabbau tutakosa nafasi yako hapa lakini wakati Mkristo anakufa tungesherekea ya kwamba ako nyumbani sasa, Imani yako imeonekana, hakuna kuteseka tena, haukna kifo tena. Nitakuambia saa hii, hanua mkristo ambaye amekufa ikiwa anaweza kurudi hapa kwa hii dunia atakubali. Ameingia mahali ambapo ni kamili, hakuna dhambi, ni furaha tele na ako pamoja na Mungu. Hii inatuomgojea wakristo wa kweli, tungetamani sana siku ile.
Lakini saa hii bado tuko hapa, tufanyaje? Vs 9 Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. Mahali yo yote, mbinguni au hapa kwa hii dunia tunataka kumpendeza Mungu. Kumbuka leo asabuhi nilitoka kutuonyesha tunaweza kujua bila shaka ikiwa tumeokoka na hii yote ni mtihani. Kitu cha kwanza ni tamaa zako, ziko wapi? Mwa vitu na watu ya hii dunia au unatamani sana kuwa pamoja na Mungu wako? Usisema unapenda Mungu na unaimba sifa zake na unahubiri neno lake lakini hutaki kuwa pamoja naye. Wakati unafikiria siku ile utakufa, unafikiriaje? Hofu, wasi wasi, unatetemeka, unaruka akili? Au ukotayari? unajua kifo ni sehemu ya maisha na ni njia ya kufika bwana wetu na kuwa na yeye. Hii mtihani si rahisi lakini ni mzuri na inaonyesha moyo wako iko wapi. Kitu cha pili ni maisha yako ni kujipendeza au kumpendeza Mungu? Mtu ambaye maisha yake ni kujipendeza ni rahisi sana kuona, angalia nje tu, angalia hii center peke yake si kama ni lazima tuende mbali, Ikiwa watu wanaangalia maisha yako, wanaona tofauti ya watu wengine? Kwa sababu mtu amnaye tamaa ya moyo wake ni kumpendeza Mungu atakuwa tofuatui kabisa kwa sababu si wengi naam na hiyo.
Kwa nini tunataka kumpendeza Mungu kila mahali kwa kila kitu? kwa sababu sisi tunajua ukweli vs.10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya. Tunajua hii siku inakuja, tunajua kila wazo, kila neno kila tendo tumefanya yote yatakuwa wazi mbele ya wote na tutalazimishwa kutoa jibu ya kwa nini. Na hii inasema sisi sote, kila mtu, mema na mabaya yote, tutatoa jibu.
Kwa sababu ya ufahamu wetu wa sisi wakristo kuhusu votu hivi tunaona mtihani ya tatu kwa vs.11 Basi tukiijua hofu ya Bwana, twawavuta wanadamu; hii neno twawavuta ni muhimu sana, tunawashawishi watu. Tunajaribu kuonyesha hawa ya kwamba hii yote kuhusu Yesu na dhambi, mbinguni na jehanamu, hukumu hii yote ni ukweli. Tunataka watu kutoka ufame wa giza na kuingia ufalme wa nuru. Hii si kazi ya viongozi au mapastor peke yao, hii ni kazi ya kila mtu mabye atasema yeye ni Mkritso. Mtiahni ya tatu ni hii, unaingea na wengine kuhusu Yesu? Usiniambia unaoenda Yesu na huwezi kuongea na mwengine kumhusu yeye. Utapost mambo mingi ya wachezaji wa michezo, waimbaji maarufu, watu maarufu, wenye siasa, nguo, viatu lakini husemi kitu kuhusu Yesu kristo? Na watu ambao wakiongea kuhusu yesu ni uongo sana kwa sababu hujasoma neno lake kujua yeye ni nani kweli kweli, vitu ambavyo vimekuwa posted si kuhusu Yesu wa bibilia. Ukitaka kujua bila shaka wewe ni Mkristo kweli kweli, waambia mwengine kuhusu Bwana wako.
Pia kwa hii mstari tuko na mtihani ingine ni uopendo wako kwa wengine. umeshika ya kwamba hukumu iko mbele ya kila mtu, watasimama mbele ya Mungu na unajaribu kuwavuta ni kuonya hawa kuhusu hii ambaye inakuja. Unapenda hawa. Usisemi unapenda Mungu lakini uko na chuki kwa ndugu yako. Nimesikia Mbubiri moja alisema ni kiasi gani tunapaswa kumchukia mtu, ili tusimwambie kuhusu ghadhabu ya Mungu iliyo mbele yake. Na ni ukweli kabisa. Hata Yohana alisema kwa waraka wa kwanza wa Yohana 4:20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Mtihani mzuri sana kutoa shaka mingi ya wokovu wako ni upendo wako kwa watu. Na upendo ukweli kwa hawa ni kuwaambia ukweli, hata uikiwa ni Baba ama mama au rafiki.
Mtihani ingine kutoa shaka yo yote ya wokovu tunapata kwa Waraka wa pili wakorintho 5:14 Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote; Hii mstari hapa ni ajabu. Paulo alisema Upendo wa Kristo watubidihsa. Anasema Upendo wa Kristo unatutawala. Wakati alisema hii ni kama amewekwa pingo na anaongozwa na hii. Mtihani kwako ni hii, upendo wa kristo inakutawala? Upendo wa hii dunia na na kujipenda ni tofuati sana na upendo wa Kristo. Upendo wa hii dunia au kujipenda ni mimi, mimi, mimi. Upendo wa Kristi ni wengine. Hata Yesu alisema amri mbili ya kutimiza torati yote ilikuwa kupenda jiarani yako kama nafsi yako. Yesu alisema kwa kitabu cha Yohana 15:12-13 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Na alifanya kama alisema Waraka wa kwanza wa Yohana 3:16 Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Mtihani ya upendo wa kristo ni hii, Unapenda watu? Unasema ndiyo, ninapenda watu, sawa, Jilianganishe na hizi mistari Wafilipi 2:3-4 Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Hi ni wewe? Ikiwa ni wewe unaweza kuishi maisha yako biula shaka yo yote ya kwamba umeokoa. Wakati upendo wa kristo unakutawala unakuwa kama hii mstari inasema Ya waraka wa pili wakoritnho 5:14b. maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote; Sababu upendo wa Kristo unakutawala ni kwa sababu umeshika ukweli wa hii yote, kila kitu kuhusu Yesu na dhambi ni milele ni ukweli na huna chaguo jingine, hii ni sababu Paulo anasema vs15. tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao. walio hai waiswe hai tena kwa ajili ya nafsi za wenyewe. Umeshika ya kwamba maisha yako si yako, huwezi ishi maisha haya kwako mwenyewe lakini yote ni kwa Yesu.
Natumaini sana unaanza kuona ukiweka Yesu akuwe kila kitu kwa maisha yako itakuwa na matokeo na ni matakeo ya ajabu hata Paulo alisema kwa vs.13 Maana ikiwa tumerukwa na akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu; au ikiwa tunazo akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu. Watu watasema wewe ni mjinga, wewe umeruka akili, kwa sababu watu wa kawaida hawawezi kufahamu vitu vya Yesu. Wakristo wa kweli wako na silaha zenye nguvu zaidi kuwahi kujulikana kwa mwanadamu, ni Upendo, Furaha, Amani, Subira, wema, upole, kiasi au kujitawala. Na tunaishi kama tunamini na watu wanashangaa! Hii ni vitu ambavyo inaonekana kwa maisha yako? Ikiwa unajibu ndiyo, kuwa na salama kwa sababu wewe ni Mkristo wa kweli.
Halafu tunafika mstari yetu ya leo Waraka wa pili wakoritnho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. Hata imekuwa, tumeona sababuPaulo alisema hii, hizi mistari zote kufika hapa na nasema mtu akiwa ndani ya Kristo. Na ikiwa vitu hivi vyote viko maishani yako, wewe ni ndani ya Kristo. Na ikiwa umekuwa ndani ya Kristo anasema umekuwa kiumbe kipya. Umebadilishwa, wewe ni mtu tofauti kabisa, moyo wako, mawazo yako, kama unaongea, kama unaamini, kama uonaongea yote ni tofauti, hutaki hata kukumbuka kama ulikuwa. Umesafishwa kabisa ndani. Ya kale yamepita. huyu ya zamani ameenda. Huyu ambaye alipenda kujipendeza, na labda alikuwa mwongo, mwizi, mwuaji, malaya, mlevi, mzinizi huyu mtu amepita na amekuwa mpya. Ni kama umezaliwa mara ya pili, umepewa nafasi ingine katika Yesu Kristo, Mungu ameweka Roho yake ndani yako. Ajabu sana! Tuko na story mingi sana kwa historia yetu ya watu ambao walikuwa wabaya zaidi kwa hii dunia, watu ambao unajua Jehanamu ni kwao na utasema hata haitoshi. Na Mungu anawaokoa na wanakuwa watu tofautiu kabisa, kiumbe kipya.
Nitakuuliza Watu amabo wanakujua, watasema hii ni wewe? Ikiwa ni ndiyo, ishi maisha yako kwa usalama kwa sababu wewe ni mkristo ukweli. Ukitaka kufanya mtihani mzuri sana, enda kwa mtu fulani ambaye wanakujua na uliza hawa, wakati unaona mimi, unaona nini? Wakisema wewe ni Mfuasi wa Ule mtu anaitwa Yesu, wewe unafuata bibilia, Bila shaka yeye ni rafiki yako kwa sababu unaongea kuhusu yeye wakati wo wote. Kuwa na amani, wewe ni Mkristo.
Tuko na siku tatu kabla ya mwaka mpya inakuwa, mimi nitasema Kama Paulo alisema kwa Waraka wa pili wakorintho 13:5 Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.7777
Isipokuwa umeanguka mtihani. Leo asabuhi fanya hii tafadhali. Usiendelea kucheza na vitu hivi, labda ni kwa sababu ya kazi yako hapa kwa mission, au msichana au kijana fulani unapenda, wachaana na hii maneno yote, milele iko mbele yetu, bado uko na uhai, kumaanisha bado uko na nafasi kuweka imani yako jatika Yesu, ni kutubu kwa dhambi zako, maishan ambaye umeishi ya kujipendeza na vitu vya hii dunia, na kuamini ya kwamba Yesu Kristo alikufa mslabani kwa ajili ya dhambi zako na kwa sababu yeye ni Mungu, alifufuka katika wafu na anaishi leo. nataka ninyi kusikia, hakuna kitu umetenda, hakuna dhambi yo yote isiyoweza kusamehewa.
Nitaomba, ukitaka kuwa kiumbe kipya leo asabuhi tuko hapa kueleza zaidi kuhusu Bwana wetu Yesu kristo. Unajua sisi ambao ni wakristo wa kweli Paulo anaendela kwa vs.20 kusema kwa hiyo, sisi ni mabalozi wa kristo, kama Mungu anasihi kupitia sisi, tunawaomba ninyi kwa niaba ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Sisi tuko hapa kama mabolozi, tunaweza kukuonyesha ukweli wa yesu kwa neno lake. Kaa mahali unaketu na tutakuja kwako au kuja hapa mbele baada ya ibada yetu na ongea na mimi. Anza hii mwaka kuwa Mkristo wa kweli, bila shaka yo yote.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu kristo Asifiwe, na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.