Followers of Christ. John 1:38-39

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 3 views
Notes
Transcript

John 1:38-39

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika 1:38-42. Tulimaliza wiki iliopita kuona Yohana Mbatizaji mara ya pili kuweka Yesu mbele ya wanafunzi wake na alisema tazama Mwana Kondoo wa Mungu. Mara ya kwanza hatujui ikiwa walishangaa au hawawezi kuamini au nini lakini mara ya pili tuliona walishika kama Yohana anasema na tulimaliza wiki ilioptia kuona wale wanafunzi wa wili wa Yohana Mbatizaji wakamfuata Yesu. Tuliona kwetu ambao ni wakristo ni walimu na ni mzuri hatukati tamaa au kufa moyo wakati watu hawashii kama tunasema kuhusu bwana wetu yesu kristo lakini lazima tuendelea kuishi imani yetu mbele ya hawa na kueleza hawa vitu vya Yesu. Kitu kiingine ni muhimu kufanya ni kuwaombea ya kwamba Mungu atafungu mawazo na macho yao kuona ukweli wake na watatubu kwa dhambi zao na kuamini hii yote ni ukweli. Ninaweza kukuambia saa hii, wnegi wenu ambao ni wakristo leo asabuhi hapa kwa kanisa letu watu wengi wamekuombea na tumeona Mungu wetu kujibu maombi ya watoto wake. leo asabuhi tumefika kwa mistari ambazo tunaona wakati mtu anaamini katika Yesu Kristo inakuwaaje.
Tusome mistar yetu ya leo kwa muktadha yao Yohana 1:35-42 Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe). Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Kumbuka wii iliopita tulisema hizi mistari tunasoma kanisa la kwanza la yesu Kristo, ilianziswa hapa. Ilikuwa Andrea na Mtume Yohana. Tunasoma vs.38 Yesu aligeuka, akamwona wakimfuata. Kumbuka wiki iliopita Wanasimama hapo na mwalimu wao yohana Mbatizaji, aliwaambia hawa huyu ni mwana kondoo wa Mungu na walimfuata. Hawajasema waacha tujaribu kupata majibu zaidi, Hawajasema waacha nikuje wiki ijayo kuona tena ikiwa ni ukweli, walifanya nini? Kwa hii mstari tunaona waliwacha Yohana Mabtizaji na walianza kufuata Yesu. Yohana Mabtizaji hajaenda na hawa na ni kama walikuwa nyuma ya Yesu wakati anatembea kwa sababu tunasoma Yesu aligeuka akmwona wakifuata. Nitauliza wewe, Mkristo, ikiwa Yesu algeuka saa hii atakuona ukimfuata? Au wewe uko wapi? Ni ajabu kufikiria Andrea na Yohana na walisikia na waliingia nyuma ya Yesu kufuata yeye bila shaka.
Wakati tunafikiria sisi ya zamani au hata watu ambao wanaketi hapa leo na hawajui yesu. Wameketi kwa kanisa mara mingi na wamesikia kuhusu Yesu walisikia jina lake lakini hawajamjua yeye, walisikia watu kuimba sifa zake hata labda walitumia mdomo wao na sauti yao kusema maneno kuhusu yesu lakini hawamjui na labda siku moja wanaketi kanisani na wanaongojea pastor, au labda walikuwa peke yao kwa chumba chao nyumbani na wanasoma neno la Mungu, au labda walikuwa peke yao na walikuwa na shida na walipiga magoti mbele ya Mungu na wanaomba kwa Mungu kusiaida hawa na kuwaonyesha Yesu Kristo kweli kweli, labda walikuwa kwa kazi na ule mtu ambaye alikuwa jina tu, yesu alifunuliwa kwao na Mungu. Walikuwa kama Ayubu wakati alisema kwa Ayubu 42:5 Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona. Sasa wameona Yesu kufanya kazi maishani yao kufungua macho yao kufungua mawazo yao kujua yeye, matokeo ya hii ni nini? Roho zao zimeamshwa, sasa wanasikia kama lazima wafanye kitu, hawawezi kuketi na kusikia lakini anaanza kutafuta huyu Yesu, kuwa na uhusiano na yeye ni kila kitu, ni tamaa ya moyo wake zaidi ya kila kitu, ni kama hii kwa Yohana na Andrea wakati walisikia kuhusu yesu. Natumaini sana ni kama hii kwako. Na tunasoma waliweka matendo kwa imani yao na walimfuata Yesu na walikuwa karibu nyuma yake.
Halafu kwa hii mstari vs.38 tunaona maneno ya kwanza ya bwana wetu Yesu kristo alisema Mnatafuta nini? Mananeo haya ni ya kwanza tunaona Yesu kusema kwa kitab cha Yohana. Muumba ta kila kitu, Mfalme wa mifalme aliuliza wale wanafunzi wawili swali ya ajabu. Hajasema untafuta nani lakini unatafuta nini. Yesu kwa sababu yeye alikuwa Mungu alihaa jua kila kitu, alijua mioyo yao na mawazo yao lakini hii ilikuwa kama mtihani kwao. Hata kwetu kwa siku zetu hii ni swali nzuri sana. Ikiwa Yesu alikuuliza unatafuta nini, utasema nini? Kwa sababu baada ya hii hapa tutaona watu wingi walianza kufuata Yesu lakini si kwa sababu walitaka ukweli, lakini kwa sababu ya vitu amabavyo watapata. Hawajataka yeye, walitaka faida ambao inakuja kwa jina la yesu lakini hawajataka yesu mwenyewe. Fikiria walimu wa uongo wa siku zetu, wanatumia jina la yesu vibaya sana, wanasema vitu hajasema kwa neno lake, wanakula watu wa Mungu sana. Wanatumia jina la Yesu lakini si kwa sababu wanataka ukweli wake lakini kwa sababu ya faida watapata. Hata wakristo wingi kwa hii dunia wanasema wanafuata Yesu lakini kwa nini? hata weswe unafuata Yesu kwa sababu gani? Kwa bibilia tunasoma walifuata yesu kwa sababu alilisha hawa, aliponyesha hawa na familia yao, walifuata yesu kwa sababu ya miujiza yake.
Ni pastor moja aliandika kitu kizuri sana na wakati ninasoma hii ni mzuri hata mahali unaketi kujipima na kujua ikiwa hii ni wewe. Alisema “Swali muhimu kwa kizazi chetu—na kwa kila kizazi—ni hili: Ikiwa ungeweza kuwa na Mbingu, bila ugonjwa, na marafiki wote uliowahi kuwa nao duniani, na vyakula vyote ambavyo umewahi kupenda, na shughuli zote za burudani. umewahi kufurahia, na uzuri wote wa asili uliowahi kuona, anasa zote za kimwili ulizowahi kuonja, na hakuna mzozo wa kibinadamu au majanga yoyote ya asili, je, ungeweza kutosheka na Mbingu, ikiwa Kristo hakuwepo?” Watu wingi wanaishi maisha yao kama jibu ni ndiyo.
Lakini bodo uko na watu kama Yohana na Andrea kwa sababu walijua Yesu ni nani na walijua hawa mwenyewe ni nani na walijua wako na hitaji kubwa kwake. Wlijua hawawezi kuendelea bila yeye na alikuwa namba one juu ya kila kitu maishani yao. Wengi kwa historia yetu walikuma kama hii na hata waliteseka sana kwa sababu ya Yesu na kumfuata yeye. Wengi walichomwa, wlikatwa kwa msumeno. vichwa vyao vilitolewa, waliraruliwa na wanyama wakali mbele ya umati mkubwa wa watu, walikufa njaa, walizunguka kwa hii dunia uchi, tunasoma kuhusu wachace wa wale kwa kitabu cha Wahebrania 11:36-38 wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi. na rudi kwa vs.38 na tunasoma kitu cha ajabu bibilia inatuambia vs.38  (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), Hii ni moyo wako wakati unafikiria Yesu? Ikiwa Yesu anakuuliza unatafuta nini jibu lako litakuwa nini? Ukijibu swahili hili ukweli inakuonyesha ukweli kuhusu roho yako na iko wapi kweli kweli.
Ni muhimu kujua sisi sote, kila mmoja moyo wake inatafuta kitu, kwa hii dunia ni mambo mawili tu, ni Yesu au kitu ambacho si Yesu, ni mali, umaarufu, urahisi na starehe, raha, ama—nini? Moyo wako umewekwa juu ya nini? Au ni tamaa za mioyo yako kujua yeye zaidi, kuwa karibu na yeye na kutembea na yeye kila siku kila dakika? Unawea kusema hata ikiwa ni kidogo kama Daudi kwa Zaburi 42:1-2 Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Ni mzuri kujipima na kuona moyo wako inatamani nini zaidi.
Rudi kwa Yohana 1:38 tunaona Yesu kuuliza wale wawili swali Mnatafuta nini na tutaona jibu lao. 1:38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? Kitu cha kwanza wanasema kwa Yesu ni Rabi. Hii neno ilitoka lugha ya Wahebrania na maana yake ilikuwa Bwana lakini kwa agano jipya ilianza kuwa Mwalimu na ilitumiwa kwa mtu ambaye alikuwa mwalimu wa torati ya Musa. Wakati walisema Rabi ilionyesha heshima kwa Yesu. Na waliuliza yeye unakaa wapi? Andrea na Yohana walitaka kujua Yesu ankaa wapi kwa sababu walitaka kuwa na yeye zaidi. Walisikia Yohana kusema Yesu ni nani, walikuwa mahali mbapo watu wingi walikuwa na walitaka kuingia na kuketi na Yesu na kuwa peke yao na bila shaka kuuliza yeye maswali mingi walikuwa nai. Yesu aliuluza hawa mnatafuta nini lakini si kitu walitaka, si baraka fulani au kuona muujiza lakini walitaka mwenye kubariki. Tena nitasema hapa nimzuri unajipima, unajiuliza kwa nini mimi ninafuata yesu. Ninataka nini? Ni kwa sababu ya kazi yangu ni kwa sababu mama na baba na familia yangu wanaenda kanisa na ni lazima mimi ninafuata Yesu? Ni kwa sababu ya baraka fulani unatafuta? Au ni kwa sababu ndani yako umevunjika, roho yako haiwezi pumzika na unajua wewe ni mwenye dhambi na umeona ni huyu mtu, Yesu ako na majibu yote na unatafuta yeye sana, kwa neno lake na kwa maombi. Ni wewe peke yako unaweza kujibu swali hili.
Vs.39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Mananeo haya ya Yesu ni tamu sana na ni kwetu sote hata leo asabuhi. Ikiwa unatafuta Yesu, ikiwa unataka kujua ikiwa yeye ni ukweli, ukitaka tumaini, amani, furaha, uzima wa milele, masama ya dhambi zako anasema njoni, na utona. Ni ajabu sana karibu kitu cha kwanza baada ya Yesu ametangazwa ya kuwa yeye ni Mwana Kondoo wa Mungu na njoni na utaona. Andrea na Yohana bila shaka walitaka hii jibu sana. Yesu amekaribisha hawa kuenda na yeye peke yao na kukaa na yeye. Bibilia haisemi mahali Yesu alikaa lakini tunaweza kuangalia mistari kama Luka 9:58 Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake. Labda Wayahudi walifikiri wakati Masihi wao atakuja atafika na hadhi ya kifalme na utukufu. Lakini Yesu bila shaka hata hajakuwa na mahali kujilaza kichwa na mahali alikuwa ilikuwa chini sana. wengine wanaandika ya kwamba hata mahali alikaa labda ni pango tu, a cave. Wakati yesu alikuja aliharibu mawazo na mipango yte ya watu na Kiyahudi kuhusu vile angekuwa. Mungu anafanya kazi yake kama hii. Mafarisayo walikuwa na pesa walifanya kazi yao hekaluni, walishi maisha mzuri sana na Mungu alikuja na anazaliwa horini na hajakuwa na mahali hata kujilaza kichwa chake na ni kwa njia yake wenye dhambi watapata wokovu. Ni ajabu. Kitu kiingine tunaona kwa Yesu kuwaambia Andrea na Yohana njoni ni kuona wema wake. Hajakuwa busy na hajasema siwezi ongea na ninyi saa hii, niko busy. Kumbuka hii ni Masihi wao, mwana wa Mungu, Mwokozi. Yohana na Andrea hawajakuwa watu muhimu, walikuwa wavuvi, maskini, na bado Yesu anasema njoni, karibu na utaona na tutaketi pamoja.
Tunaendelea kusoma kwa Yohana 1:39 Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. Sasa yesu alikaribisha hawa kuona mahali anakaa na walikubali. Nitasema hapa kwetu, Bibilia inatuambia Mungu si mabali na sisi sote. Matendo 17:27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Ikiwa Yesu Kristo alikukaribisha na alisema njoni utaenda? Ama utaendelea na maisha yako? Ni ngumu lkaini watu wingi wanamkataa kila siku na wanaendelea na maisha yao kama Yesu hana maana, Yesu anasema kwa kitabu cha Mathayo 11:28-30 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Daudi alisema kwa Zaburi 34:8 Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini. Wanasema nini? Njoni, jaribu na masiha yako itakuwa tofauti sana. Hii dunia na kila kitu ndani yake utasahau haraka sana wakati unafuata yesu.
Tunaona kwa Kitabu cha Yohana 1:39 wakakaa kwa Yesu siku ile. Tunaona ilikuwa saa kumi. Sasa tena hii inaonyesha ya kwamba huyu mtu amabye anaandika kiatbu hiki, Yoahana, alikuwa hapo hata alijua na aliandika ni saa ngapi waliingia na Yesu. Na w wailichelewa kidogo na ilikuwa jioni, walikaa na yesu mpaka asabuhi. Jaribu kufikiria ikiwa unaweza kuketi na Mungu, Muumba wa kila kitu na ilikuwa wewe na rafiki yako na yeye kwa masaa mingi. Utauliza maswali gani? Utataka kujua nini? Hatujui waliongea kuhusu nini lakini lazima ilikuwa mzuri na Mungu akipenda tutaona wiki ijayo matokeo ya kuongea na Yesu.
Leo asabuhi ikiwa hujui Yesu nataka wewe kusikia anasema njoni? Anakaribisha wewe kufuta yeye na kuamini katika yeye. Bibilia imejaa na mistari kutuambia hii. Angalia Yeremiah 29:13 Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Leo asabuhi unaweza kutubu kwa dhambi zako na kuamini na kufuata yesu au unaweza kuendelea na maisha yako na kumkataa. Ukitaka kuongea zaidi tuko hapa, tunataka sana kuongea na wewe kuhusu Bwana wetu. Tutakuwa na Wawili wanasimama uko nyuma kwa mlango, waambia unatuka kuongea kidogo au ukitaka kuongea na mimi, karibu mbele baada ya ibada yetu au unaweza kukaa kwa kiti chako na wakati wote wametoka nitakuja kwako. Lakini tafadhali usiendelea kukataa wakati Yesu anakukaribisha.
Asanteni sana, Bwana wetu yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.