Johns Testimony John 1:31-34

John  •  Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 12 views
Notes
Transcript

John 1:31-34

Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika 1:31-34. Kufika hapa tumeona mambo mingi sana. Natumiai sana ikiwa uko na shaka yo yote ya Yesu Kristo ni nani imetolewa kwa masomo yetu kufika hapa. Tumeona Yesu ni Neno, Yesu ni Muumba ya kila kitu tumeona Yesu mwokozi, Masihi, tumeona kusema ukweli Yesu kristo ni Mungu mweyewe. Kumbuka hata sababu Yohana aliandika kitabu hiki Yohana 20:34 hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Alitaka sisi kujua sana, bila shaka Yesu alikuwa Masihi wa watu wake, alitaka sisi kuamini katika yeye na kazi yake. Hii ni sababu aliandika kuhusu zaidi ya kiujiza ishirini kwa kitabu chake na ni vitu ambavyo ni Mungu peke yake anaweza kufanya. Mtume Yohana alikuwa mtu ambaye alikuwa hapo, Alikuwa shahidi wa macho, na alitaka sisi kujua Huyu anaitwa Yesu, alitembea hapa na binadamu alikuwa Mungu mweyewe. Lakini kama mtu ambaye anataka kuwasahwishi wengine Yohana alileta mashidi kuhakikisha kama anasema na mtu ya kwanza alileta ni Yohana Mbatizaji, Yesu alisema Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; Ikiwa Yesu Mwenyewe alisema hii kuhusu huyu lazima yeye ni shahidi mzuri.
Tuliona wiki iliopita Yohana Mbatizaji alisema kitu ambacho ilishangaza watu bila shaka alisema kwa vs.30 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Naam na gani? Yohana Mbatizaji alizaliwa miezi sita kabla ya Yesu. Ilikuwa kwa sababu Yesu hana mwanzo na hana mwisho. yeye ametoka katika umilele wote uliopita, kumaanisha alikuwa Mungu. Na sisi tuliangalia hii sana wiki iliopita. Sasa leo kwa mistari yetu tunaona Yohana Mbatizaji anaendelea kutuambia Yesu ni nani kweli kweli. Tunaweza kusema ni Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji.
Tusome mistari yetu ya leo. Yohana 1:31-34 Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu. Hii ni neno la Mungu wetu kuhusu Bwana wetu Yesu Kristo.
Tuombe:
Kitu cha kwanza Yohana anasema ni wala mimi sikumjua. Alijua yesu kwa sababu walikuwa familia. Lakini anamaanisha hapa hajajua yesu alikuwa Masihi mpaka alimbatiza. Anaendelea kusema kwa vs.31 lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. Yohana Mbatizaji sababu alibatiza watu na maji ilikuwa kutangaza a kwamza Masihi anakuja. Bado hajajua ni Yesu. Si kama Yesu na Yohana walikuwa pamoja na walipanga kudanganya watu. Yohana Mbatizaji alikuwa na huduma kubwa sana, wafuasi wingi sana na wakati wake alijua inaisha. Hajajaribu kuendelea kuwa kitu kubwa, alianza kuweka macho ya watu kwa Yesu Kristo. Wakati Yohana alitangaza kwa vs.29 Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu, huduma ya Yohana ilitimizwa. Kumbuka sababu ya Yohana Mbatizaji ilikuwa Kutayarisha njia ya Bwana. Tunaona kazi Yohana alifanya kabla ya Yesu alifika kwake kwa kitabu cha Mathayo 3:1-2 Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Amesema ufalme wa mbinguni umekaribia. Alijua wakati wake iko karibu kuisha, alijua sababu yake na alihubiri na aliwaambia watu kutubu kwa sababu hakuna uzima wa milele bila kutubu. Leo asabuhi hata sisi tunasema, tubu kwa dhambi zako, kwa sababu bila kutubu na kuamini hakuna uzima wa milele. Tunasoma Mathayo 3:5-6 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao. Watu wengi wanaenda kwa Yohana na wlikuwa wakiziungama dhambi zao. Hii ni watu ambao watakuwa watu wa Mungu. Yohana alisema vs.11 Ndipo walipomwendea Yerusalemu, na Uyahudi wote, na nchi zote za kandokando ya Yordani; naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao. na tunasoma vs.13 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Yesu aliingia. Ufalme wa mbinguni imefika. Sababu ya Yohana Mbatizaji ilitimizwa hata mara ingine tunasoma kuhusu Yohana Mbatizaji anapoteza kichwa chake.
Lakini rudi kwa kitabu cha Yohana kwa sababu Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji ni muhimu sana. Ni kama inaweka muhuri ya Mungu juu ya Yesu ni nani kweli kweli. Yohana 1:32 Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake.
Sasa hapa Yohana Mbatizaji anaongea kuhusu Ubatizo wa yesu. Tunaona Kwa Mathayo 3:13 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Hii ni ajabu sana. Jaribu kufikiria hii, Yohana alitangaza Yesu na alisema ni Masihi, ni Mwana Kondoo wa Mungu halafu anafika kwako na alitaka kubatizwa. Na Yohana alijibu vizuri sana tunaona kwa Mathayo 3:14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Ni watu wengi sana leo hawatakuwa na shida kubatiza Yesu kwa sababu itaonyesha hawa ni wakubwa hawa ni kitu, itasaidia huduma wao kugrow sana, utaona kwa status ya watu, lakini Yohana Mbatizaji alijua yeye ni nani na alijua Yesu ni nani na alisema, mimi ni nani? Siwezi kubatiza Masihi, kristo wa Mungu, hata ni mzuri wewe Yesu, Unibatize, lakini baada ya Yesu kuongea na Yohana alikubali na alimbatiza yesu. Sasa ni kitu hapa tunasoma Kwa Yohana 1:32 ya kwamba anasema Huyo aliniambia. Sasa ni kama Yohana Mbatizaji kwa njia ya kusikia sauti au kwa maono au ndoto, Mungu aliongea na Yohana. Na alisema Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake. ALisema huyu ni uliye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Kusema hii ni kusema huyu analeta wokovu. Na ni mtu moja anaweza kuleta wokovu kwa watu na ni Mungu. Huyu mtu ako na uwezo kupea Roho wa Mungu kwa watu.
Tunasoma kwa kitabu cha MWanzo wakati dunia ilikuwa mbaya sana, uovu, Mungu alisema kwa Mwanzo 6:3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Kwa sababu watu walikuwa wabaya sana. Mungu alitoa Roho yake kwa watu. Ni Mungu peke yake ako na uwezo kufanya hii. Halafu tunasoma kwa Ezekieli 36:26-27 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Watu waliongojea unabii huu kwa miaka mia sita na sasa inafanyika hapa kwa Yohana mbatizaji. Ni huyu mtu Yohana Anabatiza, Yesu, Alisema atawabatiza watu kwa Roho Matakatifu. Yesu mwenyewe alisem kwa kitabu cha Yohana 14:16-17 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; Yohana Mbatizaji anajua bila shaka ni huyu anaotwa Yesu Naam na gani? Mungu alimwambia yeye wakati anabatiza mtu na ataona hii kitu cha ajabu kufanyika utajua yeye ni Kristo, Masihi. NA tunasoma wakati Yohana alibatiza esu kwa Kitabu cha Mathayo 3:16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; Yohana aliona hii kufanyika. Aliona Roho akishuka juu ya Yesu na Mathayo alisema ilikuwa kama hua. Hii ndege hua, Ni ndege ya upendo na pia ya huzuni, na Mathayo, Marko, Luka na Yohana wote wanakubali waliona kitu kama hua ilikuja na iliketu juu ya Yesu wakati alibatizwa. Bibilia ni wazi kabisa hii ilikuwa Roho Mtakatifu. Sasa sitaki ninyi kutoka hapa na kona hua nje na kufikiri ni Roho Mtakatifu, lakini hapa ni kama Roho Mtakatifu alichagua kwa watu kuona. Na ilihakikisha kama Yohana Kbatizaji alisema ya kwamba wakati unaona huyu mtu utajua yeye ni Kristo yangu, yeye ni Mungu.
Hapa kwa hizi mistari mbili ya Mathayo tuko na Utatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Tuko na Yesu anabatizwa na tuko na Roho inatoka mbinguni kukaa na Yesu halafu angalia Mathayo 3:17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Baba ameongea. Hata akili zetuzetu haziwezi kuelewa hili, nini kinatokea hapa majini. Yohana Mbatizaji ako, anasimama hapo na Yesu, ameona vitu hivi alisikia hii sauti.
Teana tunaona kama Yohana Mbatizaji alisema kwa Yohana 1:33 Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. Tena Yohana anasema hajajua Yesu, si kama wamepanga mapema, si kama watu wetu wa leo wanaongea na watu na wanalipa hawa kuwa kipofu au kuwa kilema na wanasimama mbele ya watu kueka mikono juu yao na wanaanza kutembea na hata hawajakuwa na shida. Yohana anasema si naam na hiyo. Na tunaona Yeye aliyenipeleka kubatiza na maji, Huyo aliniambia. Hii inatuonyesha Yohana Mbatizaji aliongea na Mungu. Na anasema ni huyu nimeona hii yote kufanyika ni yeye anaweza kubatiza na Roho Matakatifu. Ni mafundisho mingi sana kuhusu ubatizo wa Roho Mtakatifu na ni uongo sana. Watu wanatumia Roho Mtakatifu vibaya sana, wanaita yeye kama mbwa, wanasema anafika kwa njia mingi tofauti, Fresh Fri, Maji, ujinga wingi sana, na tunaona hapa amefika kwa njia ya yesu kristo. Mungu akipenda tutarudi kwa hii mstari wiki ijayo kuangalia sana, jambo la Ubatizo wa Roho.
Vs.34 Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu. Mara mingi wakati tunasoma bibilia tunaweza kuruka mstari kama hii bila hata kushika kama inasema, na hii mstari ni muhimu sana, inatuonyesha mambo mingi. Ya kwanza anasema nimeona. Yohana hajasikia kutoka rafiki yake, hajasikia kuwa mbali naa hii yote anasema nimeona. Ni ngumu sana wakati uko na shahidi wa macho. Hata ikiwa polici wanakuja wakati shida iko karibu swali la kwanza ni nani ameona. Nani alikuwa kuona hii shida wakati ilifanyika. Hii ni mfano mzuri sana kwetu zadi kwetu wakristo usiseme uongo. Najua hapa wakati watu wanakosa kitu cha kwanzaa wanajaribu kusema ni uongo. Ulifanya hii? Hapana, Ulikuwa uko? Hapana. Ni kama kupuma kusema uongo na ni ngumu sana. Kwa wakristo bibilia inatuambia kwa Mathayo 5:37 maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu. Hi ni lazima kwa watu ambao wanasema wako nuruni, wanafuata Yesu, hata ikiwa ni ngumu. Maneno ya sisi wakristo yangekuwa ukweli kabisa na kila mtu, wasioamini wangejua ikiwa huyu amesema, ni ukweli kabisa, hakuna shaka yo yote. Ingekuwa tabia ya maisha yetu kusema ukweli, ikiwa tumekosa au kwa jambo lo lote. Tunaweza kusema neno lako ni jina lako, watu wanajua ikiwa wewe ni mkora na tabia yako ni kudanganya au wanajua ikiwa wewe unasema ukweli. Nimeona hapa mara mingi sana, watu wanapigwa simu na mtu anasema uko wapi na utasema niko karibu. Hata labda mtu anakuongojea kubeba hawa na unasema uko karibu na uko mbali sana. Uko wapi? Niko Nkoilale na kweli uko ngoswani.
Tuko na mithali moja na ni muhimu sana sisi sote tunashika umuhimu wa hii, ni Mithali 22:1 Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu. Bila jina jema hunakitu cho chote. Jina la mtu iko na dhamani juu ya dhahabu. Hii ni sababu wakati hapendi wewe kitu cha kwanza anajaribu kuharibu ni jina lako.
Yohana Mbatizaji anaendelea kusema kwa vs.34 Nimeshuhudia. Sasa jina la Yohana watu waliamini, alikuwa kali na si mtu kudanganya, ikiwa yeye anasema kitu watu walisikia, Kumbuka tulisoma ya kwamba karibu Yerusalemu wote walienda mahali alikuwa kusikia kama anasema. Na alisema Nimeshuhudia. Na ni kweli, Alishuhudia Uwepo wa Yesu, alisema alikuwa kabla yangu. Alishuhudia Ubawana wa Yesu, alikuwa sauti ya kusema nyorosheni njia ya Bwana. Alishuhudia Ukuu wa yesu alisema mimi sistahili kuilegea gidamu ya kiatu chake. Alishuhudia Kazi ya dhabihu ya Yesu, alisema Tazama Mwana Kondoo wa Mungu. Alishuhudia ukamilifu wake wa maadili alisema aliona hua kufika na kukaa juu ya Yesu. Alishuhudia haki ya Yesu ya kimungu ya kubatiza kwa Roho Mtakatifu. Na kitu cha mwisho Yohana Mbatizaji alishuhudia kuhusu Yesu ni Uwana wake wa kimungu.
Yohana Mbatizaji ni shahidi mzuri sana na kusema hii yote anasema Yesu si Mwana wa Mary tu lakini alikuwa Mwana wa Mungu mwenyewe. Baada ya hii kazi ya Yohana mabtizaji imeisha kusema ukweli, Sasa tunaanza kuona Yesu na kazi yake na yote atafanya. Na kutoka hapa mpaka mwisho ya kitabu hiki kila kitu ni kumhusu Yesu. Na Mtume Yohana anaendelea na lengo yake kutuonyesha ya kwamba Yesu ni Mungu. Tutaona Yohana kuandika kuhusu miujiza saba, na kuonyesha watu Yesu alikuwa Mwana wa Mungu na huduma wake ilikuwa ya kimungu.
Leo asabuhi umesikia neno la Mungu linashuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu, Umesikia Yohana Mbatizaji kusema Yesu ni Mungu, Umesikia Mtume Yohana kuandika Yesu ni Mungu na utasikia mimi kusema Yesu ni Mungu. Tafadhaliikiwa hujui yeye, Tubu kwa dhabi zako, Amini, weka imani yako katika yeye na yeye peke yake. Haukan njia ingine, hakuna tumaini lingine, hakuna mtu mwengine anaweza kusaidia wewe. Ni yesu tu. Labda uko hapa na una mizigo mingi sana katika maisha yako, mambo ambayo yanakuelemea nataka ninyi kusika Maneno ya Mungu kwa Zaburi 55:22 Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza. Na sikia Maneno ya Bwana wetu Yesu kristo kwa kitabu cha Mathayo 11:28-30 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. Ukifanya hii utakuwa na amani maishani yako, ukifanya hii utakuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita. Ukitaka kuongea zaidi kuhusu yesu au wokovu au dhambi maishani yako tafadhali ongea na sisi. Unaweza kuongea na mimi ukitaka, kuja hapa mbele baada ya ibada yetu au kaa kwa kiti chako na nitakuja kwako. Ikiwa unataka kuongea na mtu mwengine Kyle na Jonathan watakuwa kwa mlango wakati unatoka unaweza kumwambia hawa unataka kuongea. lakini tafadhali fikiria vitu hivi kwa sbaabu hatuna ahadi ya kesho.
Asanteni sana, bwana wetu yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.