Doctrinal Statement Pt.25 Divine Providence 2.
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 11 viewsNotes
Transcript
Divine Providence 2
Divine Providence 2
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kuhusu kama sisi tunaamini hapa kwa AIC Sekenani au Doctrinal Statement yetu. Nafikiri imekuwa wazi kwetu sote ya kwamba, kama mtu anaamini na kama ataishi maisha yake, hii ni sbabau nataka kuhakikisha sisi hapa tunaamini kama Bibilia inasema kuhusu vitu, nataka sisi kuishi maisha yetu kama watu wa Mungu wetu na neno lake ni kila kitu kwetu, ikiwa neno la Mungu linasema kitu, tunaamini, ikiwa inapinga kama tunaishi maisha yetu tubadilike, lazima tukuwe watu wa Neno. Ikiwa unasema wewe ni Mkristo na Bwana wako ni Yesu, lazima tufuate kama anasema, usiseme wewe ni Mkristo halafu unaishi maisha yako kinyume na neno la Mungu, ikiwa hii ni wewe, wewe si Mkristo, wewe ni mzushi (pretender) tu. Tumeingia hii mlango ya doctrinal statemt yetu na ni ngumu kwa watu wengi kufuata na kuamini kwa sababu watu hawajafundishwa vizuri na wamefundishwa ya kwamba, kila kitu ni kuhusu sisi, na ukweli wa neno la Mungu linasema kila kitu ni kumhusu Mungu. Yeye anatawala juu ya kila kitu, na kila kitu mema au mabaya inafanyika kwa shauri la mapenzi yake. Tumeingia Mlango wa tano na tumfika namba 2 kuhusu majaliwa ya kiungu au Divine Providence. Ni kumaanisha nini? Mungu ndiye anayetawala ulimwengu na anaingilia kati ndani yake.
Tusome namba 2: All things come to pass unchangeably and certainly in relation to the foreknowledge and decree of God, who is the first cause. Thus, nothing happens to anyone by chance or outside of God’s providence. Yet by the same providence God arranges all things to occur according to the nature of second causes, either necessarily, freely, or in response to other causes.
Namaba 2 ya kama sisi tunaamini ni muhimu sana. Mara mingi utasikia mtu kusema, huyu hana bahati, au umeshinda kitu na watu watasema huyu ako na bahati mzuri, Bahati kusema ukweli si kitu cha ukweli. Bahati ni kusema jambo lilitokea bila kupangwa au kukusudia, au bila sababu yoyote inayojulikana. Watu wengi wanaishi maisha yao naam na hii na ni uongo sana. Angalia Wakolosai 1:17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Ikiwa sisi ni wakristo wa kweli na tunafuata Neno la Mungu lazima tunaona ya kwamba kila kitu kinafanyika kwa mpango wa Mungu, si kwa bahati, si bila sababu. Sisi tunasoma Waefeso 1:11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake . Tunasoma hii na tunaona Mungu wetu anafanya kila kitu kwa kusdi lake na shauri la mapenzi yake, hakuna bahati. Si bahati umwokolewa, imepangwa tangu misingi ya dunia yamewekwa. Hakuna huyu mtu ako na bahati mbaya, hata mimi ninasema hii kucheza tu lakini hakuna kitu kama bahati mbaya, Mungu alipanga kila kitu. Mungu wa miungu, Mungu wa uumbaji ni ajabu sana. Ayubu 37:14 Sikiliza neno hili, Ee Ayubu; Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu. Leo nataka sisi kusoma mlango moja ya Ayubu, ni milango nne ya ajabu sana, lakini tutasoma moja tu, huwezi kusoma hizi milango nne na kutoka na kusema vitu vinafanyika na bahati. Mimi ninapenda sana hizi milango nne kwa sababu zinatuonyesha nguvu ya Mungu wetu na kama anafanya, vitu amabvyo sisi mara mingi Hatufikirii. Ni Ayubu 38-41 lakini sisi tutasoma 38 peke yake.
Tuanze kwa Ayubu 38:4-41 Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.
5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?
6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
7 Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
8 Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni.
9 Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,
10 Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango,
11 Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?
12 Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?
13 Yapate kuishika miisho ya nchi, Waovu wakung'utwe wakawe mbali nayo?
14 Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri, Vitu vyote vinatokea kama mavazi.
15 Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie, Na mkono ulioinuka huvunjika.
16 Je! Umeziingia chemchemi za bahari, Au umetembea mahali pa siri pa vilindi?
17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?
18 Umeyafahamu mapana ya dunia? Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.
19 Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru? Na giza pia, mahali pake ni wapi?
20 Upate kuipeleka hata mpaka wake, Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake?
21 Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo, Na hesabu ya siku zako ni kubwa!
22 Je! Umeziingia ghala za theluji, Au umeziona ghala za mvua ya mawe,
23 Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba, Kwa siku ya mapigano na vita?
24 Je! Nuru hutengwa kwa njia gani, Au upepo wa mashariki hutawanywaje juu ya nchi?
25 Ni nani aliyepasua mfereji kwa maji ya gharika, Au njia kwa umeme wa radi;
26 Kunyesha mvua juu ya nchi isiyo na watu; Juu ya jangwa asiyokaa mwanadamu;
27 Kuishibisha nchi iliyo kame na ukiwa, Na kuyameza majani yaliyo mororo?
28 Je! Mvua ina baba? Au ni nani aliyeyazaa matone ya umande?
29 Barafu ilitoka katika tumbo la nani? Na sakitu ya mbinguni ni nani aliyeizaa?
30 Maji hugandamana kama jiwe, Na uso wa vilindi huganda kwa baridi.
31 Je! Waweza kuufunga mnyororo wa Kilimia, Au kuvilegeza vifungo vya Orioni?
32 Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?
33 Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?
34 Waweza kuiinua sauti yako mpaka mawinguni, ili wingi wa maji ukufunikize?
35 Waweza kuutuma umeme, nao ukaenda, Ukakuambia, Sisi tupo hapa?
36 Je! Ni nani aliyetia hekima moyoni? Au ni nani aliyetia ufahamu rohoni?
37 Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu kwa hekima? Au ni nani awezaye kuzimimina chupa za mbinguni?
38 Wakati mavumbi yagandamanapo, Na madongoa kushikamana pamoja?
39 Je! Utamwindia simba mke mawindo? Au utashibisha njaa ya simba wachanga,
40 Waoteapo mapangoni mwao, Wakaapo mafichoni wapate kuvizia?
41 Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutanga-tanga kwa kutindikiwa na chakula?
Hata unafikiri simba anapata chakula chake kwa bahati? Hata hii imepangwa na Mungu. Unasoma kama Mungu anamwambia Ayubu na unaona ukweli wa Wakolosai 1:17 na Waefeso 1:11. Vitu vyote hushikana katika yeye na anafanya mambo yote kwa sahuri la mapenzi yake. Kama sisi tunaamini hapa hakuna kitu kinafanyika na bahati. Ingawaje kulingana na ufahamu wa kimbele na majaliwa ya Mungu, amabye ndiye chanzo cha kwanza. Hata kifo cha Yesu ilikuwa mpango wa Mungu. angalia kitabu cha Matendo 2:23 mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; Unaona? Yesu alipotolewa kwa shauri la Mungu liliokusudiwa. na anasema tangu zamani hii ilikuwa mpango ya Mungu kuokoa watu wake kutoka dhambi zao. Hakuna kitu kinashangaza Mungu, hakuna kitu yeye hajui, hakuna kitu haoni, yeye anaona mwanzo mpaka mwisho kwa sababu ni yeye ameandika kila kitu. Ikiwa sii naam na hiyo Mungu si Mungu na yeye si mwenye uwezo wote.
Hii ni sababu sisi wakristo, watoto wa Mungu tunaweza kuwa na faraja maishani yetu, tunaweza kuwa na tumaini maishani yetu kwa sababu tunajua ungu wetu anatupenda, hii ni sababu alituma Yesu kufa kwa ajili yetu na maisha yetu ni mikononi mwake. Nitatukumbusha tena ya Warumi 8:28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Hii ni vitu sisi tutasema ni mzuri na mbaya. mambo yote ni kila kitu. Ikiwa wewe ni Mkristo jifariji, uwe changamfu na simama imara.
Asanteni, kuna maswali?
