Doctrinal Statement Pt.27 Divine Providence 3a.
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 26 viewsNotes
Transcript
Divine Providence 3a.
Divine Providence 3a.
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kuhusu kama sisi tunaamini hapa kwa AIC Sekenani, ni Doctrinal Statement yetu. Kama tunaamini ni kama tutaishi. Wakati unaamini Mungu anatawala juu ya kila kitu, utaishi maisha yako tofauti kabisa, Ikiwa unaamini ni wewe onaongoza maisha yako ni wewe unatengeneza hatima yako mwenyewe, utaishi maisha yako tofauti. Hii ni sababu ni muhimu zaidi ya kila kitu tunajua na tunaoata kama tunaamini kutoka Neno la Mungu wetu, Bibilia. SI kwa pastor fulani, kanisa fulani, si mfumo fulani si kwa desturi letu au mtu yo yote mwengine. Soma Bibilia, jua bibilia na fuata kama inasema, hii ni lengo yangu kwa kanisa letu, kwa shule yetu na kwa mission yetu. SI rahisi kwa sababu wasioamini ni wingi na hawa, hawajali Mungu ni nani au neno lake linasema nini. Wengi ni wakristo wa mdomo wakati wko hapa lakini nje ya hapa hawajali Mungu. Ikiwa wewe ni Mkristo wa kweli, hii ni lazima, au labda wewe si Mkristo wa kweli. Usisemi wewe ni mkristo na unaishi maiaha yako kinyume kabisa na neno la Mungu, wewe ni mnafiki, si Mkristo.
Tumeingia mlago wa tano ya Doctrinal Statemnt yetu na ni muhimu sana kwa sababu ni kumhusu Mungu na kama anatawala juu ya kila kitu. Ni majaliwa ya kiungu. Na Mungu wetu anafanya kazi yake naam na hiyo. Wiki ilioptia tulimaliza kuangalia kama Mungu anatumia kila kitu hata maamuzi yetu na bado yote itaitimiza mapenzi yake. Hakuna kitu ni nje ya udhibiti wake, hakuna asichokijua hakuna mjabcho haoni, anajua mwanzo had mwisho.
Tusome Mlango wa tano namba 3. In his ordinary providence, God makes use of means, though he is free to work apart from them, beyond them, and contrary to them at his pleasure.
Tena wiki iliopita tuliona Mungu anaweza kutumia kitu cho chote kutimiza mapenzi na mipango yake. Leo kama tunaamini ni kama wiki iliopita ya kwamba Mungu, katika kutekeleza majaliwa ya kawaida anatumia njia na namna. Tuko na mfano mzuri ya hii kwa kitabu cha matendo. na hapa Paulo alikuwa mfungwa na anatumwa Roma kuinga mbele ya Kaisari. Siku zile hakuna gari na hakuna ndge na waliweka Paulo kwa merikebu. Kama kawaida hii ingechukua siku ishirini na tatu lakini walikuwa na shida na ilichelewesha hawa miezi tatu. Lakini walikuwa kwa merikebu na dhoruba kubwa ilikuja juu yao. Na kumbuka hii meli imejaa na wafungwa, wengi ni watu wabaya sana na wanajua wanaenda Roma kukufa. Tunajua walikuwa watu mia mbili sabini na sita kwa hii merikebu na tunafika Matendo 27:30-31 Na baharia walipotaka kukimbia na kuiacha merikebu, wakiishusha mashua baharini kana kwamba wanataka kutupa nanga za omo, Paulo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya merikebu hamtaweza kuokoka. Ni ajabu sana vs.31. Paulo bila shaka alikuwa na mono kutoka kwa Bwana ama Mungu alimwaambia hii kwa njia fulani. Hii ilikuwa majaliwa ya Munguna watu walikuwa na walipewa chaguo na tunaona baadaye walifika nchi kavu baada ya siku mingi na tunasoma vs.42-43 Shauri la askari lilikuwa kuwaua wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia. Bali akida, akitaka kumponya Paulo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe kwanza baharini, wafike nchi kavu; Lakini kumbuka Paulo alisema ikiwa wote wankaa kwa merikebu na hakuna mtu atatoka tunasoma vs.34 Basi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea. na ni ukweli kabisa kwa sababu tunasoma vs.44 Na hivyo watu wote wakapata kuifikilia nchi kavu salama. Mungu anafanya kazi yake mara mingi kama hii. Na ikiwa mtu moja alitoka siku ile labda wote wangekufa.
Tuko na mfano ingine kwa kitabu cha Isaya 55:10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; Hapa tunaona Mungu anatumia vitu kama mvua na theluji kufanya nini? kuleta maji kwa ardhi na hii maji inatumiwa na Mungu kuleta kwa watu kupanda mbegu na kwa hii mbegu watu watapata chakula. Halafu tuko na hii ahadi kubwa sana kutoka Bwana wetu kuhusu neno lake. anasema vs.11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. mungu anatumia neno lake na wakati linatumiwa tuko na hii ahadi ya kwamba haitarudi bure. Na anasema litatimiza mapenzi yake. Hiini mzuri sana kwetu kujua kwa sababu mara mingi tunaweza kufa moyo wakati tunafanya huduma wa Mungu kwa sababu tunahubiri, tunafundisha, tunongea na watu wengine kuhusu Yesu na neno lake, tunaenda kufanya uinjilisti na ni kama watu hawataki au hawasikii. Ni mzuri sisi tunakumbuka Warumi 10:17 imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
. Lakini ni mzuri sana kukumbuka hii mstari ya Isaya. Neno la Mungu halitarudi bure na itatimiza mapenzi ya Mungu. Mara mingi sisi tunafikriri hakuna mtu aliokoka leo na tumeshindwa lakini ukweli labda ni neno la Mungu linaingia huyu mtu na itachukua muda kwa Mungu kutumia hii kubadilisha mioyo ya ule mtu na pia inaweza kuwa Mungu atatumia neno lake maishani ya mtu kuleta hukumu juu yake, labda Mungu hatamwokoa huyu lakini alisikia neno na ako bila udhuru. Kwa sbabau tunajua kwa majaliwa ya Mungu neno lake halitarudi bure na itatimiza mapenzi ya Mungu.
Ni mzuri kwetu kukumbuka kazi yetu ya sisi wakristo. Hatuwezi kulzaimisha mtu kuokoa. Watu wengi wanalazimisha watu kuamini, kutubu lakini wakati tunafanya hii tunaweka mtu kuwa mkrosto wa uongo, Mungu hajatenda kazi yake kwa huyu mtu ni wewe umelazimisha yeye. Kazi yetu ni kuwa waminifu kuonyesha people ukweli wa neno la Mungu na kusihi mbele yao kama Mungu alituambia. Kumbuka Yeremiah.
Yeremiah alikuwa nabii ya Mungu na alifanya kazi kwa Mungu miaka arobaini. Nchi ya Israeli ilijaa na kuabudu sanamu na uasherati na Mungu allituma Yeremiah na neno lake kila mahali alienda kuwaonya watu kwamba wale wasiomtii Mungu watalaaniwa chini ya hukumu. Yeremiah aliitwa nabii anayelia au weeping prophet, kwa sababu ya huzuni yake ya kina na huzuni katika unabii wake. Watu wake walikuwa waovu, na alijua kwamba uharibifu ulikuwa unakuja kwa sababu ya dhambi yao. Ni ajabu kufikiri kwa miaka arobaini hakuna mtu hata moja alitubu kwa dhambi zake. Yeremiah alikuwa mwaminifu na hajaona mtu moja kuokolewa. Na Mungu alitumia uaminifu wa yeremiah kutimiza mapenzi yake.
Asanteni, Kuna maswali?
