Doctrinal Statement Pt.28 Divine Providence 3b.
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 3 viewsNotes
Transcript
Divine Providence 3b.
Divine Providence 3b.
leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa Doctrinal Statement yetu ama kama sisi hapa kwa AIC Sekenani tunaamini. Sisi tumeona mambo mingi sana. na kila jumapili ninasema hii yote ni muhimu sana kwa sababu kama unaamini ni kama utaishi maisha yako. Ikiwa unaishi tofuati ya kama unaamini wewe ni mnafiki. Lakini kusema ukweli kama tunaishi maisha yetu inaonyesha kama tunaamini kuhusu mambo mingi sana. Kwa Mkristo utaona ikiwa anaamini vitu vya bibilia kweli kweli ama anacheza kama yeye ni Mkristo. Ikiwa unaamini Mungu anachukia dhambi utajaribu sana kukaa mbala na dhambi. Ikiwa unashika ukweli wa Mungu ni nani, utafanya kama anasema kwa neno lake, utamtii kwa njia ya kufuata kama anasema. Na hii inapigana na tabia yetu, kwa sbabau tunajua tumezaliwa katika dhambi zetu na sisi ni wenye dhambi. Tabia yetu ni kujiweka juu ya maisha yetu, si Mungu, ni mimi ninatawala juu ya maisha yangu si Mungu. Ni mimi ninapanga njia na kila kitu kwa maisha yangu si Mungu. Wakati mtu ameokolewa kweli kweli anajua hii yote ni uongo na mungu anafungua macho yako kuona ukweli wake na kila kitu ni kumhusu Yeye si mimi. Ni Mungu anatawala juu ya kila kitu, hata siwezi kupumua tena leo asabuhi bila Mungu, na kujua hii nitaishi maisha yangu tofuati kabisa. Itakuwa lengo na tamaa ya moyo wangu kumpendeza Bwana wangu Yesu kristo.
Natumaini sana umeanza kuona kama sisi tunaamini kwa hii mlango ya kitabu chetu. Majaliwa ya kiungu au Divine Providence, wakati unashika ukweli wake, inabadilisha kila kitu.
Tusome kwa kitabu chetu Mlango wa tano namba 3.In his ordinary providence, God makes use of means, though he is free to work apart from them, beyond them, and contrary to them at his pleasure.
Namba 3 ni fupi sana na nilifikiri nitamaliza wiki iliopita lakini hatujamaliza. Wiki iliopita tuliona Mungu, katika kutekeleza majaliwa ya kawaida anatumia njia na namna. Tuliona hii ni vitu kama chaguzi zetu. si kama anategemea sisi lakini anaweza kutumia kutimiza mapenzi yake. Tuliona Mungu anatumia vitu kama mvua na theluji. Inanyesha na mbegu imepandwa na kwa sababu ya hii maji mbeugi inakua mpaka ni chakula na watu wanakula. Watu wingi wanasema vitu kama Mother Nature asili ya mama. Umesikia Mother nature? Ni yeye analeta hii maneno ya mvua, dhoruba, vimbunga, mafuriko, Matetemeko ya ardhi. Hii ni uongo sana. Ni mzuri unasikia saa hii Mother Nature si ukweli. Ni mzuri kwetu kubeba mistari mingi na sisi lakini kwa mambo haya ni moja ninapenda sana ni Wakolosai 1:17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. Sisi wakristo tunajua kila kitu amabcho kinafanyika iko na sababu na itatimiza mpango wa Mungu katika utoaji wake.
Lakini kama Doctrinal Statement yetu inaendelea kusema lakini anao uhuru wa kutovitumia. Kwa nini? Kwa sababu yeye ni Mungu, na kila kitu ni yake na anatawala juu ya kila kitu. Nai atamwambia Mungu hawezi kufanya kitu? Ni mzuri kurudi mstari moja na kusoma kuhusu Bwana wetu Yesu Kristo, Munu wetu Wakolosai 1:16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Vitu vyote vilumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake. Mimi, wewe, kila kitu. Na anatawala juu ya yote. Na mara kwa mara Mungu wetu atatumia vitu kupita vitu vya kawaida na hata kinyume navyo kwa mapenzi yake. Tunasoma kwa kitabu cha Hosea 1:7 Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa Bwana, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi. Kama kawaida ikiwa utaokoa nchi nzima utatumia nguvu mingi sana ya jeshi lakini hapa Mungu anafanya kitu tofauti ya kawaida Mungu aliahidi kuwaokoa Yuda “kwa Bwana, Mungu wao,” kumaanisha kwamba angewakomboa si kwa uwezo wa kijeshi au uwezo wa kibinadamu, bali kupitia uingiliaji kati Wake mwenyewe na rehema, hasa akisema kwamba wokovu wao ungetoka kwa neema ya Mungu pekee na si kutoka kwa njia yoyote ya kidunia kama vile silaha au majeshi.
Mfano ingine tunaweza kutumia ni wakati mtu ni mgonjwa sana na Madaktari wamefanya kila kitu wanaweza na hakuna dawa inasaidia na wanarudisha huyu mtu nyumbani na wanasema atakufa baada ya mwezi moja. Vitu vya kawaida ingekuwa madakatri na dawa kusiaida huyu mtu lakini Mungu anaingia na anaponyesha huyu mtu bila dawa au madaktari. Ni muujiza na Mungu alifanya kazi yake kwa mapenzi yake nje ya vitu vya kawaida. Wakati kitu kinafanyika hakuna maelezo unajua ni Mungu anafanya kazi yake nje ya vitu vya kawaida na anafanya hii kwa majliwa ya kiungu na mapenzi yake itafanyika. Ninyi unakumbuka mara mingi nimesema ni mstari moja ingine tukiweza beba na sisi kila mahali na kukumbuka kila dakika ya maisha yetu itasiaida sisi sana. Ni Matendo 17:28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. Kila kitu ni kumhusu yeye, maisha haya ni kumhusu yeye, sababu yetu ni yeye.
Halafu tunaona kwa mwisho ya namaba 3 inasema Hata majaliwa ya Mungu inaweza kuwa kinyume navyo kwa mapenzi yake, ni kumaanisha nini? Mara mingi Mungu atatumia njia na namna ambayo ni kinyume ya kawaida. Mstari yetu inatumia ni mzuri sana. Ni kitabu cha Danieli. Ninyi unakumbuka Nebukadreza alifnya dhahabu ya sanamu kubwa sana karibu meter thelathini juu na aliweka sheria kwa nchi ya kwamba wakati wanasikia sauti ya panda, na filinbi na kinubi na zeze, na santuri na zomari na namna zote za ngoma, lazima waanguke na kuiabudu hii sanamu ya dhahabu. Lakini walikuwa wayahudi ambao wamekataa kupiga magot mbele ya hii kitu. Waliitwa Shadraka, na Meshaki na Abednego. Nebukadreza alijaribu kulazimisha hawa alitoa nafasi ingine na alisema Kwa Daneli 3:15b. bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu? Ninapedna sana jibu la wale wa tatu anagalia vs.16-18 Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. Wale waliamini Mungu wao kabisa, Vs.17 inaonyesha Mungu wetu hajafungwi na mapungufu. Na wale watatu walijua hii. Lazima wote walicheka sana kusikia hii kwa sababu ikiwa unatupwa motoni utakufa. Na tunaona Nebukadreza alikasirika sana kusikia hii vs.19 ya sema alijaa ghadhabu na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto. Mara saba ni moto sana. Hata tunasoma wale amabo walishika Shadraka na Meshaki na Abednego na waliongoza hawa kwa moto walikufa kwa sababu ya moto. Shadraka, Meshaki na Abednego walitupwa motoni na tunaona kama tunaongea leo kuhusu Mungu wetu kutumia vitu kinyume vya kawaida kutimiza mapenzi yake. Angalia vs.25 Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu. alafu vs.27 Na maamiri, na manaibu, na maliwali, na mawaziri, waliokuwa wamekusanyika pamoja, wakawaona watu hao, ya kuwa ule moto ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo. Kwa sababu Mungu alifanya kinyume ya kawaida tunaona moto ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao. Sasa usijaribu hii nyumbani kwa sababu utachomeka na maisha yako yote umeona mtu kuchomwa na moto hauna nguvu juu yake? Hata nyewele za vichwa vyao hazikuteketea, hata nguo zao zilikuwa swa na ni ajabu lakini hata harufu ya moto hata kidogo haijakuwa.
Mungu wetu anafanya kazi yake naam na hiyo. Anaweza kutumia vitu vya kawaidia, au anaweza kufanya bila vitu, zaidi ya vitu na kinyume ya vitu vya kawaida kutimiza mapenzi yake. Inanichekesha wakati ninaona ay ninasikia watu kufikiri hawa wanatawala juu ya maisha yao, Kweli hajashika Mungu wetu ni nani. Lazima sisi wakristo tukuwe na ufahamu mzuri kuhusu Mungu wetu ni nani.
Asanteni, kuna maswali?