The Lords supper

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 15 views
Notes
Transcript

 
·      Kweli kweli leo ni siki siku, tumesikia ushuda wa wale na kama Yesu Amewaokoa na amebadilsha maisha yao. Kama kawaida baada ya ubatizo tunafanya meza ya Bwana. Meza ya Bwana ni kitu ambacho Yesu mwenyewe alituambia kufanya kukumbuka yeye na kila kitu amefanya kwetu. Lakini Meza ya Bwana si mchezo na tukisoma Waraka wa kwanza wakorintho 11:27-30 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. Hii inasema ni mzuri tujipime, tuangalia maisha yetu na kuhakikisha hakuna dhambi sisi tunacheza naye maishani yetu, hakikisha tukosafi mbele ya Yesu na tunatii neno lake na tunakuwa balozi yake ambaye hakuna ayibu. Anaendelea kusema vs.29-30 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala. Mimi nitaomba ikiwa uko na dhambi maishani yako ambaye hujatubu tafadhali tubu au usikunywe na usikule vitu hivi leo. Nataka kutoa dakika moja kwetu kufikiria maisha yetu, kutubu ikiwa tuko na dhambi au hata ukitaka kutoka iko sawa. Kumbuka meza ya Bwana ni kwa watu ambao wameweka imani yao katika Yesu Kristo kwa wokovu wao. Wazazi hii si kwa watoto wadogo na si kwa wasioamini.
Ikiwa uko sawa tuendelea Tusome vs 23-24 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Tukumbuke mwili wa Bwana wetu Yesu kristo alipigwa na aliteseka kwetu. Kyle and Jonathan pass out the bread. Jonathan pray (Eat the bread).
Vs.25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Tukumbuke damu ya Bwana wetu Yesu kristo ilimwagika kwa ajili ya dhambi zetu. Jonathan and Kyle pass out the juice, Kyle prays, drink the juice.
Vs.26 Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na Kumbuka wewe ni Nuru kuwa nuru ya Yesu Kristo hii wiki. Mwende salama.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.