Doctrinal Statement Pt.31 Divine Providence 4.c
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 11 viewsNotes
Transcript
Divine Provodence 4.c
Divine Provodence 4.c
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kuhusu Doctrinal Statement yetu au kama sisi hapa kwa AIC tunaamini. Tumeona ni muhimu zaidi ya kila kitu kwa sabbau kama tunaaminini kama tutaishi maisha yetu. Na pia ikiwa wewe ni Mshariki wa AIC Sekenani sisi tuna matarajio ya jinsi utakavyoishi maisha yako kwa sababu ya kile unachokiamini. Kwa mfano. Tukiona wewe unajaribu kutoa mapepo au kuponyesha watu, sisi tutakuja kwako na kusema hii ni uongo na si kama bibilia inafundisha. Ikiwa unaishi na Boyfriend au Girlfriend yako tutakuja kwako kwa sababu sisi tunaamini bibilia ni wazi kuhusu hii na ni dhambi maishani yako. Wakati wewe ni mshariki ya kanisa fulani ni kusema unaamini kama kanisa lile. Hii ni sababu kila wakati ninpigia simu ya mtu kuhusu kzai niauliza wewe unaenda kanisa gani? Ni muhimu sana kwa sababu mahali unaenda itaniambia kama unaamini na kama unaamini ni kama utaishi maisha yako na ni kama utafanay kazi yako na kila kitu. Wakati ninaongea na mtu na anasema ninaenda hii kanisa lakini mimi sijali sana, ninaweza kufanya na ninyi, kwa sababu Mungu ni moja. Mimi ninajua kitu cha kwanza viwango vyake ni vya chini au hana viwango vyovyote, hajafundishwa ukweli wa neno na labda na mara mingi ni ukweli huyu si Mkristo wa kweli. Halafu ninawaambia hawa ukikuja kufanya hapa itabadlisha maisha yako na utatoka hapa mtu tofauti kwa sababu utafundishwa ukweli wa neno.
Ninweza kukuambia leo asabuhi si makanisa mingi wanafundisha watu wao kuhusu majaliwa ya kiungu. Bila shaka wanafundisha kuhusu imani, furaha, upendo na sadaka na watu watapata hii vitu vi nne kwa mwaka mzima. Lakini hapa ninyi umewekwa na ukweli wa maandiko. Nimefurahi kuona maisha ya wengi kukomaa. Ninyi si watoto wadogo kwa imani siku hizi. Kusema ukweli umeanza tu lakini utakuwa watu kama Paulo alisema kwa Timotheo kwa Waraka wa pili watimotheo 2:15 Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. Tafadhali endelea kusoma na kujua na kufuata Yesu Kristo kwa njia ya neno lake.
Leo tunaendelea na Mllango wa tano namba 4 kwa doctrinal statement yetu. Tumekaa hapa kwa jumapili tatu lakini ni muhimu kushika ukweli ya hii. Tusome. The almighty power, unsearchable wisdom, and infinite goodness of God are so thoroughly demonstrated in his providence, that his sovereign plan includes even the first fall and every other sinful action both of angels and humans. God’s providence over sinful actions does not occur by simple permission. Instead, God most wisely and powerfully limits and in other ways arranges and governs sinful actions. Through a complex arrangement of methods he governs sinful actions to accomplish his perfectly holy purposes. Yet he does this in such a way that the sinfulness of their acts arises only from the creatures and not from God. Because God is altogether holy and righteous, he can neither originate nor approve of sin.
Tumeangalia mingi kwa hii na tumeona Mungu hata katika majaliwa yake maanguko ya kwanza ilifanyika. Hata matendo yote ya dhambi na wanadamu na malaika. Tuliona Mungu anaruhusu vitu kufanyika kwa uwezo na hekima yake na anafanya yote kwa ajili ya malengo yake matakatifu. Tuliangalia sana Ayubu na kama Mungu alipea ruhusa kwa shetani kufanya kama alifanya kwa Ayubu.
Doctrinal Statement yetu inaendelea kusema Hata hivyo, anayeleta haya, kwa njia ya kwamba udhambi wa matendo yao unatokana na viumbe vyenyewe wala sio Mungu. Sasa hatuwezi kusema Mungu alilazimisha mtu kutenda dhambi, hawezi, yeye anachukia dhambi, Mungu ni kamilifu hawezi kutenda dhambi na hawezi lazimisha mtu kutenda dhambi lakini kwa majaliwa yake ndani ya mapenzi yake anaruhusu vitu hivi. Hii inatuonyesha nguvu ya Mungu wetu na kweli kwlei anatawala juu ya yote.
Hata tuko na mifano mingi ya kwa hii kwa maandiko lakini mfano moja mzuri ni Yusufu. Kwa kitabu cha Mwanzo tuko na mlango kumi na nne, mistari 449 zinatuonyesha vizuri sana kuhusu hii majaliwa ya mungu na nitasema kwako ni mzuri uende na usome mlango wa 36-50. Inaanza na ndugu ya Yusufu wanamchukia, wanapanga kuua yeye lakini wanamwaacha shimoni kwa sababu walijua atakufa hapo. Watu Wamidiani walipata Yusufu kwa himo na walitoa yeye na alikuwa mtumwa wao, badaye wakamwuza huko Misiri, kwa Potifa, akida ya FArao, mkuu wa askari. Tunasoma mambo mingi baada ya hii na ni ajabu kama Yusufu alikuwa mtumwa, aliuzwa na Mungu alimweka katika mahali hasa alipohitaji kuwa. Farao alianza kuwa na ndoto na hakuna mtu anaweza kuifasiri. Wanaleta nani? Yusufu na Mungu alimpea uwezo kufanya hii. Badaye tunasoma Yusufu na tunafika Mwanzo 41:40-41 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Yusufu alikuwa mtumwa sasa yeye ni namba 2 kwa nchi nzima. Njaa kubwa ya miaka saba iliingia nchi ya misri na watu wote walikuja kupata chakula na ndugu wa Yusufu waliingia pia na ni story kubwa lakini baada ya mambo mingi Tunasoma kwa Mwanzo 45:5 Yusufu aanasema Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. Walimwacha Yusufu kufa shimoni, walichukia yeye sana na sasa ansema kwao ni Mungu alipanga hii na alimpeleka mbele kuhifadhi maisha ya watu. Angalia vs.8 Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri. Tena tunaona Yusufu ameshika ukweli wa Mungu wake alijua Mungu wake ako juu ya kila kitu ako na nguvu yote anasema ni Mungu alimweka hapo, ilikuwa mpango ya Mungu. Tunafika mwisho ya hii Hadithi ya Yusufu na tuko na mstari nafikiri kila mtu anajua, wakati Yusufu anaongea na ndugu zake tunapata kwa Mwanzo 50:19-20 Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.
Kama sisi tunaamini na kama Doctrinal Statement yetu inasema Mungu, ambaye kwa kuwa ni Mtakatifu na mwenye haki, siye na hawezi kuwa mwanzilishi au kukubaliana na dhambi. Hawezi lazimisha mtu kutenda dhambi, hajasema tenda dhambi, lakini yote iko ndani ya majaliwa yake na alitumia kama ndugu ya Yusufu ili kutimiza makusudi yake. Kama Mungu anafanya kwa kila kitu kila mtu na kila tendo yatatumiwa kutimiza makusudi yake. Sisi watoto wake ni mzuri tunakuwa kama Yusufu. Unafikiri ilikuwa rahisi kwa Yusufu? Ndugu zake walimchukia, walitaka kumwua lakini kwa mwishi walimwaacha shimoni kufa kwa njia ya njaa na kiu. Familia ya Yakobo hawajakuwa maskini walikuwa na mashamba na wanyama na sasa Yusufu anajipata yeye ni mtumwa na alipeleka kwa nchi ingine, na baada ya hii yote bado alikuwa mwaminifu na alimpenda Mungu, aliamini Mungu alikuwa na sababu kwa hii yote. Kama tulisoma kwa Ayubu baada ya kupoteza kila kitu alisema Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe. Hata sisi lazima tuishi maisha yetu kama hii.
Mimi sitakuwa wiki ijayo lakini hii namba tano kwa doctrinal statement yetu ni mzuri zaidi na itasaidia sisi sana kujua na kufhamu kama Mungu anafanya na sisi mara kwa mara na majaribio. Mungu akipenda na sisi tunarudi baada ya miezi tutaanaza hapo tena.
Asanteni, kuna maswali?
