To Believe, Easter 2025

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 14 views
Notes
Transcript
Leo ni siku kuu ukweli. Hakuna siku ingine ni kama hii kwetu wakristo. Leo sisi wakristo tunasherekea siku ile wakati Bwana wetu Yesu Kristo alishinda kifo na mauti. Siku hii inaleta tumaini kwetu kwa sababu tunajua hata sisi tutashinda kifo na mauti. Mimi ninsaema karibu kila wakati ninasimama mebel yenu kutubu na kuamini na kufuata Yesu kwa njia ya kutii neno lake. Kutubu nafikiri kila mtu anashika maana ya hii. Ni wakati sisi wenye dhambi tunashika ukweli ya kwamaba sisi tuko na dhambi maishani yetu na wakati Mungu anafungua macho yetu kuona ukweli wa hii tunataka kutoa hii dhambi, tunataka kuwa safi mbele ya Mungu kusema ukweli tunaanza kuchukia dhambi zetu kwa sababu Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu. Angalia Waraka wa kwanza wa Yohana 3:9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Hii nMkristo wa kweli. Na bado sisi sote tunapigana na dhambi kwa sababu bado tunaishi kwa mwili yetu na imeharibiwa na dhambi lakini Yohana anasema hapa dhambi si kitu cha kawadia kwetu siki hizi, sisi tumetubu na tunapigana na hii mwili yetu na tamaa zake. Ikiwa hii ni wewe, kweli umetubu kwa dhambi zako.
Sasa kitu cha mwisho ninasema ni kufuata Yesu kwa njia ya kufuata neno lake. Hii ni rahisi, kwa sababu tunapenda Bwana wetu na tunataka kumtii, tunafanya kama amesema na tunapata kila kitu alituambia kwa neno lake au Bibilia. Maisha yetu itakuwa tofauti sana kwa sababu tunafuata njia ingine, si njia ya dunia na tamaa zetu za ubinafsi. Hii ni msioamini kabisa, lakini sisi tunafanya kama tunafanya si kwa sababu ya sheria ya nchi fulani lakini kwa sababu ya Bwana wetu. Sisi hatuibi kwa sababu inavunja sheria peke yake lakini kwa sbabau Bibilia inasema usiibe. Sisi tunataka kupendeza Yesu na unaweza kufanya hii kwa njia moja tu, kumfuata na maisha yako kama alisema. Neno lake ni kila kitu kwetu, usiseme wewe ni Mkristo na unapenda Yesu na nimeokoka na hujui neno la mungu, wewe ni mwongo kusema hii. Tutaona kwa mkristo wakweli maisha tofauti, Munu ametupea Roho yake ili tunaweza kufungua neno lake na kuifahamu. Ninawaambia wanafunzi wetu, ukitaka kukaa mjinga kwa vitu vya Roho, acha bibilia yako juu ya meza imefungwa. Sisi wakweli tutapenda neno la Mungu, tutajua neno la Mungu na tutaishi kama inasema.
Sasa hutafanaya kitu cha kwanza au kitu cha mwisho bila kufanya kitu cha pili na hii ni kuamini. Na ni hii watu wanachafua sana. Kama watu watasema hapa ni ajabu, uko na watu wanajaribu kusema wameamini kwa sababu ya pastor yao aliwaombea, Wamemwagwa na mafuta ya fresh fri, wazazi wao ni wakristo, anaenda kanisa, anatoa pesa kwa sadaka, aliomba sali fulani siku moja, mambo mingi sana na kama kawaida hata huwezi kusikia kuhusu Yesu. Leo kwa hii siku ya pasaka nataka sisi kushika maana ya kuamini na sisi tunaamini nini exactly. Bila kuamini kama tutaona leo, wewe si Mkristo na bado unaishi dhambini na siku moja utaingia hukumu bila tumiani lo lote.
Sisi tunajua Hii siku ya Pasaka ni siku kubwa sana kwa Wakristo. Bila siku hii, sisi tuko na shida, kwa sababu Mwokozi wetu bado ako kaburini. Yeye hajafufuka. Wakati sisi tunaongea na wengine kuhusu Yesu Kristo bila shaka tunaongea kuhusu tumaini letu, na tumaini letu ni Yesu alishinda Kifo na Mauti. Ikiwa wewe ni mtu bila tumkaini nataka wewe kusikia liko hapa kwa Yesu kristo. Hata kifo hajashinda yeye na alifufuka kwa sababu yeyey ni Mungu na kuonyesha sisi sote ambao tutaweka imani yetu katika yeye hakuna kitu na hakuna mtu na hakuna mungu mwengine anawea kufanya kama yeye.
Tusome mistrai yetu ya leo waraka wa kwanza wakorintho 15:55-57 kuko wapi, ewe mauti, kushinda kwako? Uko wapi, ewe mauti, uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Hii ni neno la Mungu wetu kuhusu ufufuo wa bwana wetu yesu kristo.
Tuombe:
Kwa Mkristo huwezi kusikia maneno tamu Zaidi ya hii. Nani ameshinda mauti? Unajua mtu mwengine, au miungu mingine ameshinda mauti? Mohamed amefufuka? Buddha amefufuka? Mariamu mama ya Yesu amefufuka? Hawa walishinda kifo na mauti? Bado hawa wakokaburini. Hata watu wengi wanaenda kwa kaburi ya miungu yao na bado wanaabudu hawa. Nataka ninyi kujua ikiwa mtu amekufa na ako kaburini, hawezi kusikia mambi yako, hawezi kusaidia wewe hata hakuweza kujisaidia. Na saa hii kila kaburi ya wale ni mifupa ndani hakuna uhai, wale wote wameingia hukumuni kusimama mbele ya Mungu wa miungu ya mfalme wa mifalme na walisimama hapo biloa tumaini. Ni Yesu tu amefufuka na anaishi leo, Nani ni kama Bwana wetu? Hakuna. Sasa kwetu wakristo hakuna hofu, Shetani hana mamlaka juu yetu kwa sababu tunajua Mungu wetu ameshinda dhambi na ameshinda kifo na mauti. Sisi tunaweza kuishi maishia yetu bila wasi wasi.  
Yesu alikuja, alitumwa na Mungu kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Yuda Alimsaliti Yesu usiku moja na askari walimshika Yesu. Walimpeleka mbele ya kila mtu ambaye walikuwa na mamlaka, serikali yote. Moja alisema hakuna kitu kibaya ndani ya huyu mtu lakini makuhani makuu walipiga kilele sana na walisema Msulubishe, Msulubishe, Pilato alisema kwa desturi lao mfungwa moja anaweza kuenda, na aliuliza hawa watu wanataka nani kutoka? Walisema utufungulie Baraba. Hii ni ajabu sana. Nani anajua maana ya jina la Baraba? Ni ajabu kwa sababu wakati watu wale walipiga kilele na sauti kubwa walisema utufungulie kwetu, Baraba. Maana ya Baraba ni Mwana wa Baba. Walisema utufungulie kwetu Mwana wa Baba. Lakini hawajaona mbele ya Macho yao kweli kweli, Yesu ni Mwana wa Baba. Ni ajabu sana. Kumbuka hata kwa masomo yetu kwa kitabu cha Yohana tuliona wakati Yesu alibatizwa na alipanda kutoka majini tulisoma kwa kitabu cha Mathayo 3:17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Yesu alikuwa Mwana wa Baba Mungu lakini wale kwa ujinga na dhambi zao hawawezi kuona.
Pilato alikubali na Yesu alienda msalabani. Lakini kwanza walimpiga yeye sana, halafu alibeba msalaba wake kwa mlima, inaitwa Golgotha. Walifika Golgotha na aliweka msalaba yake chini na walimweka yeye juu ya msalaba. Waliweka msamari kwa miguu yake na mikono yake. Kwa nini? Kwa sababu warumi walijua kuua watu sana, walikuwa mafundi kwa hiyo kazi, na walijua wakati walifanya hii na unashikwa na miguu na mikono ni ngumu sana kupumua. Ni lazima wakati unapamua mwili wako inaenda juu na uzito wako iko kwa misumari kwa mkono na miguu yako. Inaleta uchungu sana. Yesu anatoa damu sana, haiwezi kupumua rahisi na alikuwa msalabani kwa kila mtu kuona. Ni mzuri kukumbuka, kwa nini. Yesu alifanya hii yote kwa sababu gani? Ni kwetu, Kila mtu hapa leo, ukiamini. Na pia ni kwa kila mtu ambaye wataishi duniani wakati wo wote, wakiamini. Kutubu, kuamini na kutii neno lake. Ukiamini kama tulisema saa hii, utakuwa mtu tofauti, utakuwa kiumbe kipya.
Wanafunzi wake bila shaka waliogopa sana na walikimbia. Bwana wao akokaribu kufa. Wanafikria nini? Wewe utafikiriaje ikiwa ni wewe? Umetoka kial kitu, umefuata huyu mtu ambaye unafikiri ni Masihi, ni Mungu wako na sasa amepigwa sana, anatoa damu na ako kwa msalabani mbele ya wote, hakuna shaka kwaqo sasa huyu mtu anaitwa Yesu atakufa.
Angalia Yohana 19:30 Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake. Imkwisha. Wakati tunasema lazima unaamini haya maneno ya Yesu ni muhimu sana. Yesu alimanisha nini? Mwana Kondoo wa Mungu alichukuiaye dhambi za ulimwengu, Shetani ameshindwa kabisa, Bei ya dhambi imelipwa kwa watu wa Mungu, Watu ambao wataamini na kuweka imani yao katika yeye. Ukombozi ulitimia. Watu wanatolewa kutoka ufalme wa giza na wameletwa kwa ufalme wa nuru, uzima wa milele unapatikana, amani, furaha, tumaini limekuwa.
Tunaona kitu cha ajabu inafanyika kwa cha Luka 23:44-45 Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hadi saa tisa, jua limepungua nuru yake, pazia la hekalu litapasuka kati kati. Halafu Yesu alikufa. Hii ni muhimu sana. Kitu cha kwanza tunaona ni ilikuwa giza kabisa saa ngapi? Saa sita mpaka saa tisa. Hii ilionyesha nguvu ya Mungu juu ya umbaji wake. Mahali ingine bibliani inasema hata dunia ilitetemeka. Lakini pazia la hekalu lilipasuka. Maana ya hii nini? Nani anaweza kuingina hekalu nyuma ya pazia? Makuhani tu. Kama leo kwa wakatholiki. Unaingia chumba kidogo kuongea na mkuhani, na yeye anaongea na Mungu kwa ajili yako. Siku ile wakati Yesu alikufa Biblia inatuambia pazia lilipasuka. Maana ya hii ni, sisi tunaweza kufika Mungu peke yetu sasa. Hakuna mahitaji ya makuhani au mtu Fulani kuongea na Mungu kwako, wewe unaweza. Si pastor yako kuongea na Mungu kwako, wewe unaweza. Hii ni habari njeema sana. Kila mahali, wakati wo wote, wewe unaweza kuongea na Mungu, Imekwisha, na hii ilikuwa ishara ya kwamba kifo cha Yesu imerudisha uhusiano kati ya Mwanadamu na Mungu ulirejeshwa. Lakini lazima kuamini.
Baada ya hii tunasoma walitoa mwili wa Yesu, na walimweka kaburini. Bila shaka wanafunzi wake wamejificha, maisha yao ni fujo. Walifuata huyu na sasa amekufa, sasa nini? Bila shaka walifikiri tufanyaje? Bwana wetu amekufa. Na ni kweli walimwona Yesu msalabani na waliona alikufa.
Angalia Luka 24:1-7 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu. Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta; nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu.
Tunaona siku ya kwanza ya Juma. Hii ni siku gani? Ni Jumatatu? Ni jumapili. Hii ni sababu sisi wakristo tunafanya ibada yetu jumapili, kwa sababu Bwana wetu alifufuka, siku gani? Jumapili. Na tunaona siku ya kwanza wanawake walikuja na walileta manukato (Spices) kuweka kwa mwili wa Yesu. Wakati walifika waliona jiwe limetoka mahali yake. Na hii jiwe si kitu kidogo. lilikuwa kubwa, na mzito yake lilikuwa kama 1-2 tons. Ni mzito sana. Wanawake wanaona imetoka mahali yake, na waliingina lakini hawajaona mwili wa Yesu. Bila shaka mafikiro yao yalikuwa mtu fulani ameiba mwili wa Yesu. Halafu tunasoma wanaume wa wili walisimama uko na nguo zao zilikuwa mara dati sana, kama nuru. Sisi tunajua walikuwa malaika. Lakini wanawake hawajajua hiyo.
Na wanaume waliuliza swali nzuri sana, walisema Kwa nini mnatafuta aliye hai katika wafu?  Bila shaka wakati walisikia hii walishangaa. Waliona yeye msalabani na waliona yeye alikufa. Sasa wanasikia hii. Halafu wanasema vs.6 Hayupo hapa, amefufuka. Maneno haya nii maneno tamu Zaidi ya kila kitu unweza kusikia. Bwana wako amefufuka. Sasa kila kitu Yesu amewaambia hawa walianza kukumbuka. Imani yao bila shaka illikua sana. Vs.6 waliendelea kusema Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa bado yuko Galilaya. Akisema, imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulubiwa, na kufufuka siku ya tatu. Walikumbusha hawa maneno ya Yesu. Yesu mara mingi alimwambia hawa atakufa na baada ya siku tatu atafufuka. Lakini hawajashika kama anasema. Sasa siku ile imefika. Vs.8 ya sema Wakayakumbuka maneno yake.
Watu wengi hata leo wanasema hii ni adithi tu. Wengi wanajaribu kusema Wanafunzi wa Yesu waliiba mwili wake na wanafunzi wake walisema alifufuka. Madini mengi hata Waislamu wanasema hii si ukweli. Yesu hajafufuka. Lakini Waraka wa kwanza wakorintho 15:6 inatuambia baada ya Yesu alifufuka aliwatokea ndugu Zaidi ya mia tano pamoja. Watu wengi walimwona Yesu baada ya alifufuka. Hii si watu wachache. Ni ngumu kudanganya watu mia tano.
Tunakumbuka adithi Ya Tomasi. Yeye alikuwa na shaka kwamaba Yesu alifufuka na Yesu alisimama mbele yake na Tomasi alimwona, na Yesu alisema weka kidole chako kwa shimo ya mkono wangu. Tomasi alisema Bwana wangu na Mungu wangu. Aliamini. Kumbuka pia alitembea na wa wili kwa bara bara ya Emau.  Yesu alikuwa hapa duniani siku arobaini baada ya alifufuka. Aliongea na wengi. Mimi ninaweza kusema Yesu alifufuka siku ile, Yesu anaishi leo, Anaketi kando ya Baba yake. Na siku moja anarudi tena.
Kweli kweli habari njeema si Yesu alikufa msalabani. Habari njema ni kifo na mauti wameshindwa kushika Yesu hawawezi kushinda yeye. Yesu amefufuka, na Yesu ameshinda kifo na mauti, hii ni habari njema ukweli. Tafadhali ishi maisha yako naam na hiyo. Ishi maisha yako kama Yesu anarudi siku moja, Ishi masiha yako kama Yesu anaketi kando ya Mungu na anaona kila kitu. Ishi Maisha yako bila ayibu, Ongea na wengine kuhusu ufufuo wa Yesu na waambia hawa anaishi leo.
Hakuna kitu kwa dunia inaweza kuleta tumaini kama hii. Wakati unalala kitandani chako usiku, unaweza kulala salama kwa sababu Yesu amefufuka. Wakati shida inaingia maisha yako, uko na tumaini kwa sababu Yesu amefufuka.
Maisha ya wakristo ni hii, Yesu amefufuka. Bila hii, Hakuna wakristo kwa sababu Bwana wetu amekufa na bado ako kaburini. Lakini sisi tunajua amefufuka na sisi tunataka watu kujua sisi ni wakristo, na ikiwa unakuwa mkristo utakuwa na tumaini kwa sababu Yesu amefufuka. Biblia inasema kwa waraka wa pili wakorintho 4:10 siku zote twabeba katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa yesu nao udhihirishwe katika miili yetu. Sisi ni balozi ya yesu, tunaongea kuhusu kifo chake kwa sababu ya ufufuo wake. Bwana wetu si kaburini, yeye anaishi!
Ikiwa wewe unataka hii tumaini maishani yako unaweza kupata. Unaweza kuwa na Amani, unaweza kujua siku moja hata wewe utafufuka na utakuwa na maisha ya milele mbinguni, pamoja na Yesu. Nafikiri kila mtu anataka hii, sivyo? Hii zawadi iko, sasa ni wewe kuamini na kuweka Imani yako katika Yesu. Kwangu mimi nawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. Usifikiri nitafanya hii kesho au wiki ijayo, ikiwa wewe hujaweka Imani yako katika Yesu Kristo ukohatarini sana. Milele iko mbele ya kila mtu, sisi hatujui kesho hata hatujui baada ya dakika moja. Nimesikia hadithi mingi sana ya watu ambao wanaketi na wanaongea na wengine, wako sawa kabisa halafu wanatoka na wako na mshtuko wa moyo, wanakufa hapo hapo. Sisi hatujui meble yetu, tafadhali usiongoja. Weka Imani yako, kabisa katika Yesu Kristo.
Biblia inasema kutubu kwa dhambi zako na ukimkiri Yesu na kinywa chako ya kuwa yeye ni Bwana na unaamini moyoni mwako Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Hakuna kitu kingine.
Tafadhali ukitaka kufanya hii, ongea na sisi baada ya ibada yetu, unaweza kuja hapa meele na ongea na mimi au kaa kwa kiti chako na nitakuja kwako lakini ninaomba, tafadhali usiendelea hata dakika moja zaidi bila kujua Yesu kristo na kutubu na kuamini na kufuata yeye.
Asanteni Sana, Bwana weu yesu Kristo amefufuka. Karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.