Christ’s First Miracle Pt.3 John 2:9-11
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 4 viewsNotes
Transcript
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika 2:9-12. Kufika hapa kwa wiki mbili tumeangalia sana muujiza ya kwanza ya Yesu Kristo. Imekuwa ajabu sana. Kwa mlango ya kwanza tuliona Yohana kutumabia Yesu na Mungu hata alileta Yohana Mbatizaji kuwa mshaidi ya Yesu ni nani kweli kweli. Sasa hapa kwa mlango wa pili anatuonyesha kwa matendo ya Yesu, ya kwamba yeye ni Mungu, na anafanya vitu ambavyo hakuna mtu anaweza kufanya, ni mungu peke yake. Kumbuka lengo ya Yohana kuandika kitabu chake, Yohana 20:31 hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Baada ya kusoma hii yote na kuona hii yote watu watakuwa bila uduhuru kuhusu Yesu ni nani, na ikiwa hujatubu kwa dhambi zako na kuamini, kuweka imani yako katika Yesu na kufuata yeye, utasimama hukumuni bila tumaini lo lote, bila udhuru wo wote. Umeambiwa, umeonyeshwa, ikiwa huwezi kuamini baada ya hii yote tuko na usemi kwa kiingereza inasema: If your gonna be dumb you better be tough, kama utakuwa mjinga, bora uwe mgumu. Shida ya vitu hivi si kama vitu vya kawaida, na wakati umekufa, nafasi imeisha, hakuna kujaribu tena, hakuna nafasi ya pili na kwa milele na milele utateseka kwa sababu ulikataa kuamini. Na tumaini umeona umuhimu wa kitabu hiki ya Yohana na sababu aliandika, yeye alijua ni nini inaongojea watu ambao hawatatubu, hawataamini, hawatafuata Yesu, Sisi wakristoi wa kweli tunajua ukweli wa nini inaongojea wale amabo watakufa bila Yesu. Si mchezo kwa sababu milele iko mbele ya sisi sote. Hata sisi wakati tunasoma kitabu hiki ya Yohana, lengo yangu kama Yohana ni kwenu kuona Yesu Kristo ni nani na utaona yeye ni Kristo, hakuna tumaini kwa mtu mwengine au kitu kiingine kwa maisha haya na maisha ambaye inakuja, na kuamini yeye ni Mwana wa Mungu na kupata uzima kwa jina lake.
Kwangu mimi sitaki ukuwe mtu mwenye maadili mema, hii haitakusaidia wakati unasimama mbele ya Mungu. Ni Yesu pekee atakusaidia. Kwangu nataka kuona moyo wako kubadilishwa, macho yako kufunguliwa na hii ikifanyika, itabadilisha maisha yako kwa sababu ni Yesu peke anaweza kufanya hii. Unaweza kuja kanisa jumapili kwa sababu ni sheria ya mission na ukifanya kazi hapa tunaomba ufike, lakini baada ya kaisa unaweza kutoka na kuvuta bangi au kukunywa pombe mpaka utalewa. Sasa natumaini sana unaona wewe hujabadilika, bado wewe ni msioamini na hukumu inakuja kwako. Tamaa ya moyo wangu ni Yesu atafungua macho yako kuona ukweli na kutok ktika mtego wa ibilisi.
Leo tunaendelea kuona muujiza ya kwanza ya Yesu na matokeo yake. Kufika hapa tunajua Yesu na wanafunzi wake na hata mama yake walikuwa kwa arusi na siku zile ilikuwa sherehe ya siku mingi na walikuwa na shida, divai imeisha. Hii ni shida kubwa, aibu kwa familia ya Bwana harusi haitatoka na hata anaweza kupelekwa kortini kwa sababu ya hii. Lakini Yesu aliingia na tuliona wiki iliopita aliwaambia watumishi kujaza mabalasi sita na maji mpaka juu kabisa. na walifanya kama alisema na yesu alisema tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Ilikuwa hapa kwa mananeo haya muujiza ilifanyika, bila kusema, maji kuwa divia, hajaguza hii maji pia, lakini kwa mapenzi yake tu alibadilisha hii maji kuwa divai na tuliosoma wote ambao wako walimtii yesu na walifanya kila kitu alisema.
Tusome mistari yetu ya leo. Yohana 2:9-11 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Tuombe:
Vs.9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, Hapa tuko ushuhuda Mwingine Yohana analeta kwa kitabu chake. Ni huyu Mkuu wa meza. Hajajua nini iliendelea na Mabalasi na Yesu kusema jaza mpaka juu. Hajaongea na Watumishi na hajaongea na Yesu na walileta hii kwake kuonja. Na ni hapa sisi tunaona muujiza ya Yesu ni ukweli. Tunasoma yale maji yaliopata kuwa divai. Na tunasoma wala asijue ilikotoka. Tena hii haijakuwa mpango na Yesu na watu kujairbu kudanganya watu, na hata huyu alishangaa kwa sababu alijua ako na shida kwa sababu hajapanga vizuri na divai imeisha. Lakini tunasoma watumishi walijua, wale walioyateka yale maji. Bila shaka imani yao ilikuwa, wale watumishi walikuwa na hawajakuwa watu wakubwa, hawajakuwa watu wa maana au muhimu katika jamii. Na Yesu alifanya muujiza yake ya kwanza mbele ya hawa. Ni mzuri kwetu kukumbuka, kama tunaona hapa, si watu wa juu na wa muhimu wanajua kama Yesu anafanya. Hata mama ya Yesu ni kama alijaribu kulazimisha Yesu kufanya kitu, mkuu wa meza hajajua Yesu anafanya nini, lakini watu ambao walikuwa chini, nyenyekevu walijua kama Yesu anafanya na Yesu alitumia hawa. Ni hawa walibarikiwa kuona na kuwa hapo wakati Yesu alifanya hii. Watumishi wa Yesu ni wale ambao ni nyenyekevu na wako karibu na Bwana wao, wanamtegemea na Yesu alisema kwa Yohana 12:26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Tunaona labda mkuu wa meza alifikiri bwana arusi alimdanganya kwa sababu anamwita na tunasoma vs.10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa. Kama kawaida kwa hizi sherehe watu walianza na divai safi na wakati walikunywa zaidi kwa siku mingi walianza kuleta ile divai ambaye ilikuwa na maji zaidi kwa sababu ya bei ya divai safi. Pia tuko na picha mzuri sana hapa ni njia ya binadamu na hii dunia au shetani na njia ya Mungu. Hii dunia na shetani wanaweka kila kitu mzuri mbele ya watu kwanza, unapata tamaa zako saa hii na ni tamu sana lakini badaye inakuwa dhaifu na mbaya. Kwanza anasa za dhambi kwa muda na kisha mshahara wa dhambi. Lakin kwa Mungu ni kinyume sana, Mungu kama tunasoma kwa agano la kale, anawaleta watu wake nyikani kabla hajawaleta katika nchi ya hadi. Kwetu wakristo ni msalaba kwanza halafu taji. nataka ninyi kusikia saa hii labda uko nyikani, na maisha ni ngumu na hata uko karibu kuchoka lakini siku inakuja ya furaha. Sikia Mitahli 4:18 njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu. Mchana inakuja kwetu wakristo. Vumilia, simama imara.
Tunaweza kuona kwa hii mstari kwa wasioamini wako na Mvinyo wao. Furaha ya hii dunia na tamaa za mwili zinatoka haraka. Labda uko na marafiki mingi, labda uko na pesa na mashamba na mali mingi na siku moja itakuja utajipata divai imeisha. Nitasema kwako weka macho yako kwa Yesu kwa sababu ni yeye tu anaweza kuleta divai njema, ni yeye tu, anayeweza kukata kiu ya moyo, Ni bei gani tunalipa kupata hii? Ni kutubu na kuamini.
Kitu kiingine ni mzuri tunaona kwa hii mstari ni mambo ya kuwnya pombe ni dhambi. Bwana wetu Yesu kristo alifanya muujiza yake ya kwanza hapa na ni kugeuza maji kuwa divai. Mimi sitaki watu kunywa kwa sababu hawajui wakati inatosha na tamaa za mwili zinaanza kuingia lakini Yesu alileta hii divai safi kabisa kw ahii sherehe ya watu wingi, sisi hatuwezi kusema kunywa ni dhambi. Kumbuka tunda moja ya Roho ni kiasi, self control. Bila hii unaonyesha wewe huna Roho Mtakatifu anaishi ndani yako kweli kweli.
Vs.11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. Sasa tunaona matokeo ya Mwanzo ua wa ishara Yesu alifanya ilikuwa na vitu mbili, kitu cha kwanza akaudhihirisha utukufu wake. Aliweka mungu wake kwenye maonyesho. Tunaona pia hii ilikuwa muujiza ya kwanza ya Yesu. Wingi wanajaribu kusema wakati alikuwa mdogo au kijana alifanya maajabu, lakini kwa maandiko sisi tunaona muujiza huu wa kugeuza maji kuwa divai ilikuwa ya kwanza kwa Yesu. Wakati Yesu alifanya muujiza haijakuwa ya kuonyesha kuruma yake tu lakini ilikuwa kuonyesha yeye ni nani kweli kweli, yeye ni Mungu. Hata leo wakati watu wanasema wanafanya miujza, hata hawa kufanya hii vitu vinatuoyesha hawa ni nani kweli kweli, ni fake na ni uongo. Usidanganywa. Ni kitu kiingine ni mzuri sisi tunashika, Ishara, miujiza na maajabu, hata vitu hivi labda haziwezi kuwashawishi watu kuamini katika bwana na injili. Hakuna mahali tunasoma wale watumishi ambao walikuwa hapo na waliona hii yote, hatusomi waliamini, hatusomi walifuata Yesu baada ya hii. Ni ajabu sana kusema ukweli kama tunasoma ni kama Yesu alitoka kana kama aliingia na wanafunzi wake, na tunajua walikuwa Andrea, Yohana, Nathanaeli na Petro. Wengie waliona Yesu kufanya muujiza lakini walikosa kuona yeye ni Masihi.
Kama Shetani anafanya na wasioamini wote, anazipofusha akili zao. Angalia Waraka wa pili wakorintho 4:4 ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Ikiwa wewe ni msioamini saa hii ni mzuri kujua hii ni wewe, Shetani amepofusha fikira zako, hata huwezi kuona ukweli, huwezi kuona nuru ya injili na utukufu wa Kristo, kwa kila mtu wako kwa community yetu, nchi yetu dunia yetu na hwawa ni wasioamini ni kama hii, Hii ni sababu sisi tunaingia na tuko naneno la Mungu na inaleta nuru kwa kila kitu, sisi tunaongea na wengine kuhusu Yesu na anaanza kubadilisha mioyo yao na kufungua macho yao, walikuwa kipofu na sasa wanaanza kuona.
Tunasoma mwisho ya Yohana 2:11 Nao wanafunzi wake wakamwamini. Sasa hi sii kusema Andrea, Yohana, Nathanaeli na Petro imani yao ilianza hapa kama aliamini kwanza hapa, lakini wakati waliona hii waliamaini sana, imani yao ilikua sana. Walisikia maneno ya Yoahna Mbatizaji, Walisiia maneno ya Yesu Mwenyewe sasa walikuwa hapo na waliona na macho yao Yesu kufanya muujiza, hii ni kusema imani yao ilihakikishwa. Hii ni sababu Yohana aliandika kuhusu hii muujiza na si hii muujiza peke yake lakini hii barua yake yote. Tumesoma karibu kila wiki sababu Yohana alandika kitabu chake lakini angalia Yohana 20:30 kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Yohana hapa anasema Yesu alifanya ishara au miujiza mingi sana na hata hakuna mtu waliandika, hawajasema ni nini. Lakini anagalia tena vs.31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Sisi mbele yetu kwa bibiia yetu tunao uthibitisho kwamba Yesu ni Mungu. Ninaomba, Amini! Nataka kila mtu kupata uzima lakini inakuja kwa njia moja na ni jina la Yesu.
Matendo 4:12 hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Ni Yesu. Nitakuuliza leo asabuhi nini kinakuzuia? Uko hapa leo asabuhi, hii ni mwanzo mzuri, lakini labda umekuja miaka mingi kuketi hapa kanisani na bado hujaamini kweli kweli. Ni baraka ya Mungu bado hujakufa, bado unapumua, bado nafasi ikio kutubu kwa dhambi zako na kuamini na kufuata yesu kwa njia ya kutii neo lake. Hii dunia na shetani na mwili yetu inataka kutudanganya sana, hii yote inatuambia si lazima unaamini, hata wanasema si ukweli lakini bado uko na time, ishi maisha yako kupata tamaa zako, jipendeza, jifurahisha na ukweli ni hii na ni mzuri unasikia kuhusu mtu ambaye ni kama watu wingi na hajali Mungu na maisha yake iko sawa na pesa ni mingi na kila kitu anataka iko na tunapata kuhusu huyu mtu kwa kitabu cha Luka 12:16-21 Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu. Hii inatuambia mingi ndani yake lakini natumaini hujakosa vs.20 Mungu akamwambia, Mbumbavu wewe, usiku huu roho yako inatakwa kutoka kwako. Anakufa! na wakati anakufa mambo yote ya hii dunia hazinamaana, ni kitu moja tu atakuwa na maana wakati hii siku inafika kwetu sote na ni Yesu.
Leo asabuhi tafadhali waachana kujidanganya, toka chini ya hii uongo wa hii dunia na Shetani na mwili wako na tubu kwa dhambi zako na amini Yesu Kristo. Ikiwa hujui kufanya hii au unataka kuongea zaidi sisi tuko hapa. Ikiwa unataka kuongea na mimi nitaomba baada ya ibada yetu ukae kwa kiti chako na wakati watu wametoka nitakuja kwako na tutaongea zaidi.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu Kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.