Cleansing the Temple John 2:12-17
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 4 viewsNotes
Transcript
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika 2:12-17. Tuliona kwa wiki tatu vs.1-11 muujiza y kwanza ya Yesu. Alikuwa kwa arusi kwa mahali inaitwa Kana na divai iliisha na walikuwa na watu wingi na ingekuwa aibu kubwa sana kwa famila ya Bwana arusi na Yesu, bila kuguza, bila kuongea na maji alibadiisha maji kuwa divai. Yohana kuandika kuhusu hii inatimiza lengo lake kuandika kitabu hiki, Yohana 20:31 hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Hii muujiza ya kwanza ilionyesha Yesu alikuwa Mungu na hata kwa mapenzi yake, vitu vinaweza kubadilishwa.
Tuliona kwa mwisho wanafunzi wake wakamwamini. Imani yao ilihakikishwa sana. Kama sisi wakati tunatembea na Yesu na tunaona kazi yake maishani yetu au maishani ya wengine, au tunakumbuka kama tulikuwa zamani na tunaona maisha yetu saa hii na kama tumebadilka na tunajua ni kwa sababu ya Yesu na kufuata neno lake, imani yetu inahakikishwa sana.
Leo tutaona Yesu na kazi yake imeanza. Tusome mistari yetu ya leo kwa Yohana 2:12-17 Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi.Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.
Tunaona kwa Vs.12 Baada ya hayo, baada ya hayo ni hii yote tumeona kwa wiki mingi kwa arusi kwa Kana na alibadilisha maji kuwa divai. Tunaona watu walienda na yeye ni Mama yake, na wanafunzi wake na walienda mpaka Kapernaumu. Sasa hii ni muhimu sana. Kapernaumu ilikuwa kama mahali Yesu alifanya kazi yake, kama Ofici yao. Pia Kapernaumu ilikuwa karibu na bahari ya Gailiaya. Watu wengi tofauti walikuwa hapo, Wayahudi, Mataifa, wasafiri, pia ilikuwa nyumbani kwa Petro, Andrea, Yakobo na Yohana. Kwa sababu Kapernaumu ilikuwa na watu wengi na Yesu kuenda uko inatuonyesha anatoka maisha yake ya kawaida na anaingia huduma hadharani. Pia tunasoma kwa kitabu cha Isaya 9:1-2 Lakini yeye aliyekuwa katika dhiki hatakosa changamko. Hapo kwanza aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na njia ya bahari; ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa. Watu wale waliokwenda katika giza Wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza. Kapernaumu ilikuwa kwa Galiaya, Yohana alishaa sema kwa 1:4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Hapa kwa Yesu kuenda Kapernaumu inatimiza unabii ya Isaya.
Vs.13 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu, Hii ilikuwa sherehe kukumbuka wakati Mungu alipowakomboa watu wake kutoka misiri. Labda unakumbuka ilikuwa pigo la mwisho Bwana alipomwua kwa malaika wa kifo chake, mzaliwa wa kwanza wa Wamisiri, lakini akazipita nyumba za Israeli. Ilisherekea kila mwaka kwa terehe kumi na nne ya mwezi wa tatu au nne. Kama sisi tunasherekea pasaka karibu na ile terehe na mwezi. na siku ile kati ya saa tisha na saa kumi na mbili walichinga kondoo wingi na walikula. Yesu alienda kwa Yerusalemu kuingia hii sherehe.
Sasa wakati yesu alifika tunasoma Vs.14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. Sasa wakati Yesu alifika kwa hii sherehe aliona kwa hekalu kitu ambacho ilikuwa mbaya sana. Kumbuka Hekalu ilikuwa mahali mbapo kwa miaka mia sita, wayahudi waliabudu Mungu, Ilikuwa ishara ya uwepo wa Mungu ya alikuwa kati ya watu wake. Ilikuwa kati kati ya kila kitu kwa myahudi kwa mambo ya dini lao. Na Yesu aliona hekalu ilikuwa soko. Amepata watu wanauza wanyama na hata watu kuvunja fedha wameketu hapo. Wayahudi kutoka kila area walikuja kwa hii sherehe. Kwa wale wayahudi ambao walikuwa wenyeji kwa Yerusalemu hii ilikuwa nafasi kubwa kwa hawa kufanya biashara na kupata pesa mingi. Wayahudi wengine walisafiri kutoka mbali kufika na kuleta wanyama kwa dhabihu ingekuwa ngumu sana. Wale walikuwa wanauza wanyama kwa bei ya juu sana. Wale wengine wanavunja fedha ni kubadilisha pesa, kwa sababu pesa ya watu kutoka mbali ilikuwa tofauti na kila myahudi ambaye alikuwa miaka ishirini na juu alilipa kila mwaka ushuru wa hekalu, na pesa walitaka ilikuwa sarafu za kiyahudi au tyrian. Watu kubadilisha pesa walikuwa na wanatoa rate mbaya sana ili wanaweza kupata pesa mingi. ikiwa tulifika na tuliona tutafikiri ni soko kubwa, huwezi kujua ni sherehe kusherekea Mungu na yote alifanya. Hii yote wakati ilianza ilikuwa mzuri na ilisaidia watu lakini viongozi wa wayahudi, makuhani wakuu, walichafua sana na walianza kupata pesa mingi. Sasa dini ilikuwa kitu cha nje, kuhusu vitu na mali kama Yesu alisema kwa Mathayo 21:13 Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.
Ukiangalia siku zetu, hii ni kila mahali, karibu kila kanisa ni mchango kila jumapili, mapastor wanalazimisha watu wao kutoa pesa kwao au wanyama au kusaidia hawa kununua gari au kujenga nyumba. Wameweka nyumba ya Mungu kuwa biashara na imekuwa pango la wanyang’anyi. Kusema ukweli kanisa si kumhusu Mungu siku zetu, ni kuhusu Man of God na mahitaji yake. Mahali watu wanakuja kuabudu Mungu wao imekuwa mahali ya soko. Ni aibu kubwa sana. Kwa nini watu wengi wanataka kuwa mapastor siku zetu? Ni kwa sababu watateseka kwa injili ya Yesu, kwa sababu watasimama imara juu ya ukweli wa neno la Mungu na watu watawachukia hata familiaa yao watafukuza hawa kwa nyumba? Ni kwa sababu labda watapigwa, au watakufa kwa ajili ya Yesu? Ama ni kwa sababu wanaona nafasi kupata pesa, wanaweza kuwa mtu mkubwa na kuwa na mamalaka juu ya watuna kujaza tumbo lake na pesa ya kundi la Mungu. Hii imefanyika siku ile kwa hekalu kama inafanyika kwa siku zetu. Ni mzuri tunaona jibu la Yesu.
Vs.15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; Tunaona Yesu ahapa kama hatuoni yeye mahali ingine. Yesu alijua usafi wa ibada hekaluni lilikuwa jambo la heshima kwa Mungu. Tunaona Yesu akafanya kikoto cha kambaa. Bila shaka yesu alichukua kamba watu wanatumia kufunga wanyama. Na tunasoma alianza kutoa wote katika hekalu. Sasa tuko na watu wengi wameandika kuhusu hii na utashangaa kujua mtu moja aliandika karibu kondoo mia mbili hamsini walichinjwa kwa hii sherehe na kondoo moja ililisha watu kumi, ukihesabu hii ni watu millioni mbili na elfu mia tano walikuwa kwa hii sherehe. Mtu wengine alisema labda hii ni watu wengi lakini bado yeye anafikiri watu walikuwa karibu elfu mia sita. Sasa hii ni kama Narok county mzima walikuwa pamoja kwa sherehe.
Shamba la hekalu ilikuwa acre 35, na mahali hekaluni watu wanauza vitu ni sehemu inaitwa mahakama ya mataifa na hii sehemu inaweza kubeba watu elfu sabini na tano. Kwa wale amabo wanafanya biashara wanasema labda watu mia mbili walikuwa na meza ya kuuza vitu. Na hapa tunasoma Yesu alifukuza hawa wote, hawa ya biashara. Lazima matendo ya Yesu iliweka macho yote kwake. Alifukuza wale wa biashara na tunasoma na kondoo na ng’ombe. Sasa fikiria mtu anajaribu kutoa wanyama wote kwa hii area kubwa. Na baada ya kufanya hii alirudi kwa wale amabo wanavunja fedha na tunaona akazipindua meza zao. Ikiwa ulikuja uko ingekuwa fujo. Watu wote wanaangalia yesu na pesa inalala chini, wanyama wamefukuzwa, lazima watu wameshangaa kabisa.
Tunasoma vs.16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. Kwa torati ya Musa ni sadaka fulani walitumia njiwa hata tunasoma kwa mambo ya walawi 5:7 Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea Bwana hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa. Ikiwa mtu hana uwezi kununua kondoo anaweza kutmia njiwa kwa sadaka yake. Maskini walikuwa wingi siku zile na wale wa biashara walijua wanaweza kupata pesa mzuri kuuza njiwa kwa wale. Si kama bei ya kondoo laini bado waliweka bei juu. Na hii kitu ilikuwa lazima, ikiwa umefika kwa hekalu kuingia hii sherehe lazima ulileta sadaka yako na ilikuwa njiwa au mnyama fulani. Yesu alitoa hawa pia na anasema kitu cha ajabu hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. yesu anasema nini hapa? Anasema Mungu ni baba yake. Hii ilikuwa shida kubwa zaidi. Lakini Yesu wmenyewe anahakikisha yeye alikuwa Masihi, Baba yake alikuwa Baba Mungu. Yesu anasafisha nyumba ya baba yake na ibada chafu. Ni haki yake kufanya hii.
Lakini ni mzuri kuuliza kwa nini Yesu alifanya hii? KWa sababu Yesu hapendi na hataki ibada chafu kwa jina lake na jina la Baba yake.Ukiangalia siku zetu hii ujinga wote inafanyika kwa kanisa na kanisa siku hizi ni mahali watu wanaona ni ya Mungu, ni ya Yesu, ni mahali sisi wakristo tunakuja pamoja kuabudu Mungu wetu, na ukiangalia kweli kweli imekuwa biashara. Ni mzuri kuuliza Yesu atafanya nini akiingia makanisa mingi ya siku zetu? Atafukuza watu? atazipindua meza? Atafurahi, atapendezwa kama watu wanaongoza watu wale na wanasema hii yote ni kwa Yesu? Atafurahi kusikia Bwana Asifiwe? Atafurahi kusikia watu wanamwagwa na fresh fri? Atapendezwa kuona kama Mapastors wanatumia watu wao, kutembea juu yao, kulzaimisha hawa kufanya vitu? Mimi sitaki kuwa ule mtu hukumuni, lazima tunajitahidi kwa yote tuliyo nayo kufanya ibada yetu kama alivyotuonyesha kwa neno lake.
Ni mzuri sisi sote tunaangalia ndani ya mioyo yetu, tujipime, Watu wengi wanajiita Mkristo na tabia yao ni mbaya kama wale wayahudi. Nataka ninyi kujua na kusikia wakati tunafanya kama wale, inmkera kabisa Bwana wetu. Ni mzuri tukumbuke maneno ya Sulemani aliandika kwa kitabu cha Mhubiri 5:1 Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya. Chunga sana.
Rudi kwa Yohana 2:17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila. Sasa kumbuka ako pamoja na wanafunzi wake na hawa wanaona hii yote inafanyika mbele ya macho yao. Hawa walijua agano la kale sana kwa sababu ilikuwa bibiia yao, walijua Masihi wao atakuwa naam na gani kwa sababu walijua agano la kale na tunasoma walikumbuka kama imeandikwa. Wivu wa nyumba yako utanilia. Wanafunzi wa yesu walikumbuka wakati Daudi aliandika kuhusu Masihi ambaye atakuja Zaburi 69:9 wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata. Yesu alijitolea kwa utakatifu kamili wa Mungu. Aliona hii yote inafanyika kwa nyumba ya baba yake na alijua watu wanatumia jina na nyumba ya baba yake kwa madhumuni ya wenyewe. Hawajakuwa kwa sababu ya Mungu, walikuwa kwa sababu ya pesa na biashara.
Kwa wakati wetu ni mzuri kukumbuka hizi mistari na kama Yesu anafikiri kuhusu watu ambao watafanya hii kwa nyumba ya Mungu, mahali ambapo Mungu anaabudiwa. Kwangu mimi, nitakuambia ikiwa uko na mapastor kwa simu yako na wanapigia simu yako au wanakutuma messages ya kutuma pesa kwao, toa namba zao, usiende kwa kanisa lao kwa sababu wanakula wewe na kusema ukweli hakuna kuabudu Mungu. Kusema ukweli kwangu, nitasema ikiwa wewe ni pastor hata usishugulike na pesa za kanisa. Usihesabu sadaka, hata ni mzuri kiongozi au mtu mwengine anafanya hii kazi. Kazi ako ni kuchunga na kufundisha kundi la Mungu. Ukitaka kujua mara kwa mara ikiwa pesa iko kwa account, uliza ule mtu ambaye anajua, wewe kaa mbali, ikiwa wewwe ni Pastor, usikutana na msichana au mwanamke kwa ofici yako peke yenu, ikiwa ni lazima kuwa nje mbele ya wato wote lakini nitasema kuwa na bibi yako pamoja nawe. Chunga sana kazi Mungu amekupea, hata sisi sote ambao ni wakristo, Mungu ni baba yetu pia na ni mzuri tukuwe na moyo kama Yesu kuchunga nyumba ya baba yake. Ni kazi yetu ya wachungaji kwanza.
Leo tumeona tena Yohana kuandika vitu kuhusu Yesu ambavyo vinatuonyesha Yesu alikuwa Masihi ukweli, hata aliita Mungu baba yake, watu walishangaa. Tutaona wiki ijayo Mungu akipenda, jibu la wayahudi kwa hii maneni yote nakama wataongea na Yesu.
Asanteni Sana, Bwana wetu Yesu kristo Asifiwe na karibuni wiki ijayo.