Jesus, our sanctuary John 2:18-22

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 10 views
Notes
Transcript
Leo asabuhi tunaendelea na maomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika 2:18-22. Kwa wiki chache tumeona Yesu kuingia hekalu na aliona kama watu wanafanya hekaluni na waliweka nyumba ya Baba yake, nyumba ya Mungu wetu kuwa mahali ya biashara. Si ngumu kuangalia leo na kuona makanisa mingi sana wamekuwa mahali ya biashara. Swali nzuri kuuliza ikiwa Yesu aliingia kanisa lako atafanyaje? Atapendezwa na kusema tunaleta sifa na utukufu kwa jina lake au tunachafua jina lake mbele ya dunia na tunatumia jina lake kudanganya watu na kuapata pesa. Tuliona Yesu kuingia siku ile na alianza kufukuza watu na kupindua meza ya wale ambao wanadabilisha pesa. Ilikuwa kali sana lakini hata kwa hii Yesu hajatenda dhambi. Na tulimaliza wiki iliopita kuona wanafunzi wa Yesu walikumbuka kama iliandikwa kwa agano la kale kuhusu Masihi ambao atakuja Wivu wa nyumba yako utanilia.
Lazima kwa hii yote wingi wanaangalia Yesu wakati alifanya hii hekaluni na lazima ilileta maswali mingi na tutaona maswali na Yesu kuongea na viongozi kwa mistari yetu ya leo.
Tusome Yohana 2:18-22 Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya? Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha. Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu? Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake. Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe
Ikiwa unaweza kujiweka uko siku ile bila shaka ungeshangaa kabisa. Hata labda wewe ungesema nini inaendelea hapa. Na tunaona vs.18 Wayahudi wakajibu. Wayahudi hapa ni Polici ya hekalu. Lazima hii maneno yote ilifika masikio ya viongozi wa wayahudi na walituma Maafisa wao kuangalia. Maafisa walifika na lazima waliona fujo kila mahali, wanyama wanakimbia, pesa inalal chini kila mahali na wanasema vs.18 Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya? Si kama wanauliza swali lakini wanapinga mamlaka yake. Yesu aliingia na hajajali mamlaka ya wale ambao wanafanya vitu hivi kwa hekalu na yeye mwenyewe alileta ukweli kwa nyumba ya baba yake. Kwa sababu ni hekalu, wale polici walitaka kujua ikiwa yesu anaweza kuonyesha hawa ishara ya miujiza kuonyesha yeye ako na mamlaka kufanya kama alivyofanya. Kwa macho ya wayahudi ni nabii ya Mungu anaweza kufanya kama Yesu alifanya. Na sisi tunajua Yesu alikuwa nabii kuu, lakini Yesu alianza huduma yake na wale hawajajua yeye ni nani. Kitu kiingine tunaona kwa hii maneno yote, bado hawajashika Yesu. Kama Yesu alifanya labda walifikiri alikuwa mtu ambaye alikuwa mamlaka.
Wayahudi mara mingi waliuliza kwa ishara na shida ni macho yao yamefungwa, macho ya kiroho. Kwa sababu Yesu kufanya hii kwa hekau iikuwa wazi kabisa ya kwamba Mungu alikuwa na ujumbe kwa ajili yao. Wanauliza ishara, iko mbele ya hawa lakini hawakukubali kamwe zile walizopewa. Tutasoma badaye Yohana kusema kwa Yohana 12:37 Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini; Ni kama watu wa siku zetu. Wanasema, nitamini Mungu akifanya hii ama hii na Mungu anafanya mambo mingi hata maishani ya ule mtu na hawawezi kuona kwa sababu wako wafu. Moyoni ni ngumu. Siku zetu kusema ukweli hakuna tofuati ya siku za Yesu. Ni mzuri kujua bila macho ya kiroho huwezi kuona vitu vya Mungu, bila Roho Mtakatifu kuishi ndano yako huwezi kufahamu kama Mungu anafanya. Ikiwa wewe unaishi kwa shaka au huwezi kushika ni mzuri kuuliza ikiwa moyo na macho yako yamefunguliwa na Mungu.
Yesu anasimama mbele ya wale, Yesu, Mwana wa Mungu, Masihi wao na kama tuliona kwa mlango wa kwanza walimkataa. Na Yesu alisema kitu cha ajabu kabisa na lazima polici na wayahudi wote hata wanafunzi wake walishangaa kwa vs.19 Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.