Being Born Again John 3:4-6
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 16 viewsNotes
Transcript
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika 3:4-6 . Tulimaliza wiki iklopita kuona Yesu kusema Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Hii sentenci moja ni muhimu sana na kukosa maana yake, mtu anaweza kukosa uzima wa milele. Kumbuka kama ulimhubiri ya zamani alisema kuhusu Hizi mistari “MAZUNGUMZO kati ya Kristo na Nikodemo, yanayoanza na Hizi mistari, ni mojawapo ya vifungu muhimu zaidi katika Biblia nzima. Hakuna mahali pengine popote ambapo tunapata maneno yenye nguvu zaidi kuhusu watu hao wawili wenye nguvu, kuzaliwa upya, na wokovu kwa imani katika Mwana wa Mungu. Mtumishi wa Kristo atafanya vyema kujifahamisha kabisa na sura hii. Mtu anaweza kuwa hajui mambo mengi katika dini, na bado akaokoka. Lakini kutojua mambo yanayoshughulikiwa katika sura hii, ni kuwa katika njia pana inayoongoza kwenye maangamizo.” hii ni ukweli kabisa.
Kumbuka tuliona Nikodemo ni nani na kufika kwa Yesu kwake haijakuwa kitu kidogo na alikuja kwa usiku. Bila shaka Yesu kumwambia Nikodemo vitu hivi ilimshangaza. Maisha yake yote Nikodemo alifuata sheria sana, alijua taratibu zote za ibada yao. Alikuwa kwa mafarisayo kumbuka kwa wakati ya Yesu walikuwa Mafarisayo karibu elfu sita. na Nikodemo alikuwa hata mkubwa ndani ya hii, alikuwa Sanhedrin, wale walikuwa sabini na moja, lazima kufika hapo alifuata sana kila kitu ya dini la Wayahudi. na Wayahudi walikuwa watu wa Mungu, walifikiri. Kama Yesu alisema kwake hapa ni kuwaachana na vitu vile vyote na kuanza tena. Kwa nini? Kwa sababu mfumo mzima wa Nikodemo ulijengwa juu ya haki ya matendo, na ilikuwa kwa matedno yake Nikodemo aliweka tumaini lake na haijakuwa na nguvu ya kumwokoa.
Kusema ukweli ni kama watu wengi wa siku zetu, wanaeeka tumaini lao kwa matendo yao, kwa familia walizaliwa, kwa serikali yao, kwa baba yao kwa sababu yeye ni pastor, kwa kaisna lao kwa sababu wanendea uko kila jumapili. Sasa Fikiria Nikodemo, Yesu anasema kwake, kwa sababu yeye ni myahudi si kumaanisha ataingia ufalme wa Mungu, kwa sababu alikuwa mfarisayo na watu waliona yeye ni mtakatifu zaidi ya wengine, haina maana, kuwa Sanhedrin, haina maana , ako na Yesu mbele yake na anamwambia Nikodemo bado hajaokoka na hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Ni mzuri sisi oste tunasikia leo asabuhi kama Nikodemo alisikia, Kila kitu amabcho tumeweka tumaini letu ambao sisi tumefanya kuokoka ni bila maana. Hii ni ajabu sana. Leo tutaona jibu la Nikodemo kusikia hii na Yesu kuendelea kueleza zaidi kuhusu kuzaliwa mara ya pili.
Tusome mistari yetu ya leo Yohana 3:4-6 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Sasa kitu cha umuhimu sana nataka sisi kushika. Wakati Yesu anasema Mtu asipozaliwa mara ya pili, ni mzuri sisi tunashika maana ya kuzaliwa mara ya pili, kitu cha kwanza ni kumaanisha, maabadiliko. Lazima wakati mtu anaokoka kweli kweli maisha yake itakuwa tofauti. Si madaliko ya nje ya maadili, au nje, ni mabadiliko kamili ya mapenzi ya moyo na taba yako. Kusema ukweli umefufuka, umekuwa kiumbe kipya, umetoka mauti sasa uko na uhai. Pia uko na asili mpya, tabia mpya za maisha, ladha mpya, tamaa mpya, maamuzi mapya, maoni mapya, matumaini mapya na hofu mpya. Hili ndilo lilio katika kuzaliwa upya, kuzaliwa mara ya pili. na hii yote si kazi ya mwanadamu bali ya Mungu.
Tunaweza kuona kwa jibu la Nikodemo, hajashika kama nimesema saa hii na kama Yesu alimwambia. Vs.4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Swali la Nikodemo linatuonyesha ya kwamba Nikodemo haajkuwa na macho ya roho. Alikuwa Mwalimu wa Israeli, alikuwa mkubwa kwa dini la Wayahudi lakini, hajakuwa na Roho Mtakatifu kuishi ndani yake, hajashika kama Yesu anasema. Hata Mtume Paulo anatuambia kwa Waraka wa kwanzaq wakorintho 2:14 mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Paulo anatuonyesha hata shida ya Nikodemo, hajashika kwa sababu hajakuwa na Roho Mtakatifu. Roho hajafanya kazi yake ndani ya Nikodemo. Siku zetu tuko na watu wengi zaidi, wanajua jina la Yesu, wanaweza labda kueleza kuhusu Yesu, labda ni mwalimu au pastor, lakini Roho hajafanya kazi yake ndani ya huyu mtu na hajabadilishwa. Sitaki ninyi kujidanganya. Maarifa juu ya Yesu hayaokoi mtu. Kuenda kanisa, hakumwokoi mtu, Kutangaza injili ya Yesu, si kumaanisha ule mtu ameokoka. Bado wale watu hawajazaliwa mara ya pili na wakati umezaliwa mara ya pili, Roho Mtakatifu anaishi ndani yako na unaishi tofuati kwa sababu wewe ni kiumbe kipya na ufahamu wako kuhusu mambo mingi ni tofuati kwa sababu unaweza kusoma, na kufahamu kama neno la Mungu linasema.
Haqpa kwa Nikodemo alikuwa kipofu kwa vitu vya Roho. Yesu amesema hapa kwa Nikodemo lazima aanze tena. Kuingia ufalme wa Mungu si kuongeza kitu kiingine kwa orodha yake ya matendo amefanya, lakini kuwaachana na kila kitu ameweka tumaini lake na kuanza tena. Pia ni mzuri tunaona kama Nikodemo alifahamu yesu kusema, kuingia tumbo la mama yake tena, haiwezikana. Ni mumaanisha kuingia ufalme wa Mungu ni kitu ambacho Mungu mwenyewe anaweza kufanya kwa mtu.
Katika mazungumzo haya kati ya Yesu na Nikodemo, ni mojawapo ya sehemu ya Maandiko ya kushangaza kuhusu wokovu. Tuko na Nikodemo na kuangalia yeye tutasema bila shaka yeye ni Mtu wa Mungu, alikuwa kuwa na kila kitu nje kuonyesha yeye ni mtu wa Mungu. Mafarisayo wote walikuwa kama hii, hata yesu aliwaambia wanafunzi wake kuhusu Mafarisayo kwa kitabu cha Mathayo 23:3 yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi. Kwa mambo ya nje, kwa utaratibu, huwezi kushinda mfarisayo. Hata Yesu anasema kila kitu wanakuambia myashike na kuyatenda kwa sababu kama wanasema ni ukweli. Hata Yesu alisema kwa Mathayo 5:20 nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Kama walisema ilikuwa juu sana lakini shida ni kama alisema mfano wa matendo yao msitende, maana wao hunena lakini hawatendi. Kwa nini? Kwa sababu hawawezi, hawana Roho anaishi ndani yao, na bila ROho Mtakatifu huwezi kuishi kama neno la Mungu linasema. Angalia kama Mafarisayo ya wakati wetu na ni mapastor, angalia wanachosema na angalia wanachofanya. Kila siku kuna kashfa (scandal) nyingine maishani yaoamabo tunasoma kwa news au television. Wanapenda msimamo wao kuwa pastor lakini ndani hawa ni wafu, bila Roho ya Mungu. Hapa Yesu alimpa changamoto Myahudi Nikodemo aliyeshika dini sana, kukiri kuwa alikuwa amefilisika (he was bankrupt) kiroho. Ni kusema hakuna roho ndani yake, na akamwambia aache kila kitu alichokuwa anakitumaina kwa ajili ya wokovu.
Leo asabuhi tunasoma maneno haya ya Yesu na nitasema kwako, waachana na kila kitu ambacho unaweka tuamini lako na weka kwa Yesu pekee. Paulo tena alituonyesha njia ya kufanya kama Yesu anasema. Angalia Wafilipi 3:8-9 nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; Unapomfikiria Yesu, Unapofikiria kumfuata Kristo, je, hivi ndivyo unavyofikiri? Jipima, ikiwa unafikiri kitu tofauti nitasema kwako kutubu na kumwamini Yesu pekee.
Turudi kwa Yohana na tunagalia jibu la Yesu kwa Nikodmeo wakati alisema nitarudi kwa tumbo la mama yangu? Vs.5
Ni kitu kiingine nataka sisi kuona kwa hii mstari yetu kwa Yohana 3:4.
