Principles for Worship Pt.2

Sermon  •  Submitted   •  Presented
0 ratings
· 21 views
Notes
Transcript
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kuhusu kanisa na kanuni ambazo kwazo kanisa la Kristo, lazima lifanye kazi. Tumeona kanisa ni nini na ni nani, tuliona kanuni mbili tofauti watu wanatumia kufanya ibada yao. Moja ilikuwa kanuni ya kawaida au normative principle, na ingine ilikuwa kanuni ya Udhibiti au Rugulative Principle.
Tuliona Kanuni ya kawaida inatumiwa kwa makanisa mingi siku zetu na hii ni sababu tuko na mambo mingi inafanyika kwa makanisa yetu ya leo. Kumbuka maana ya hii kanuni ilikuwa wazo kwamba desturi au kipengele chochote ambacho hakijakatazwa waziwazi katika Maandiko kinaruhusiwa katika ibada za ushirika. Kanuni hiyo inaruhusu utendaji mbalimbali, kuanzia maonyesho yenye drama hadi matangazo na ala za muziki za kisasa, mradi tu hazipingani na Neno la Mungu na zinatumika katika kulijenga kutaniko. Ni kusema ikiwa neno la Mungu haijakataza kitu unaweza kufanya. Mara mingi sana tunaona desturi linaanza kuingia kanisa kwa sababu ya hii, wanaanza kujali hisia ya watu na uzoefu wao kuliko ukweli wa neno la Mungu. Ni mzuri tena ninatukumbusha ya kwamba tuko hapa leo asabuhi kuabudu Mungu, kila kitu tunafanya ni kwake, si kwetu.
Kanuni ya pili ilikuwa kanuni ya udhibiti au Regulative Principle. Maana ya hii ni Mungu analikataza kanisa kutekeleza kipengele chochote cha ibada isipokuwa zile anazoziweka waziwazi katika maandiko. Kwa jumla huwezi kuenda nje ya neno la Mungu na kufanya kama unataka kumwabudu. Mungu mwenyewe ameweka kwa neno lake kama anastahili kuabudiwa. Wakati sisi tunaenda nje ya neno lake ni kama sisi kusema tunajua zaidi ya Mungu, sisi tunajua afadhali.
Leo asabuhi nataka sisi kuona kwa neno la Mungu, jinsi anavyotaka kuabudiwa na nini kinafaa katika ibada. Kumbuka mstari yetu kwa hii masomo yetu na tunapata kwa Waraka wa kwanza watimotheo 3:15 upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Nataka kuendelea kidogo kuangalia mistari ambazo zinatuambia kuhusu umuhimu wa ibada yetu. Tulianza wiki iliopita lakini wakati wetu umekwisha. Paulo aliandika kwa kanisa la Kolosai na tunaona ibada yao ilianza kutoka kama Paulo aliwaonyesha. Kitabu cha Wakolosai 2:18 Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili; Hapa tunaona Paulo kuwaambia hawa waacha kusikia wengine na kama wanasema kufanya vitu. Hata tunasoma waliabudu malaika. Walikuwa na watu ambao waliingia kanisa kusema walikuwa na maono na Paulo anasema hii ni kujivuna bure. Paulo anasema sisi wakristo wa kweli tumekufa pamoja na Kristo na kwa vitu vya hii dunia angalia vs.20 Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Aliuliza swali nzuri sana kwa nini kujitia chini ya amri na kama tunaishi duniani. Hii ni mambo ya desturi iliingia kanisani. Kama nini? Angalia vs.21 Msishike, msionje, msiguse; Hii ni nini? Fikiria watu amabo wanasema hawa ni wakristo laikini wanakunywa chai yao tofauti, mambo ya majani au kama ilipikwa, Au watu amabo wanasema hawakuli hii ama hii, siwezi kula nguruwe, si wezi kula nyama, na wanasema kwa sababu ya dini lao. Pauoo hapa anasema hii ni amri ya wanadamu si ya Mungu. Vs.22 Paulo alisema hii yote ni mafundisho ya wanadamu. Vs.23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe. Sisis hapa hatutaki kufanya hii, tunataka kufuata neno la Mungu si amri au mafundisho ya wanadamu. Kumbuka siku moja utasimama mbele ya Mungu kutoa majibu, utasema nini?
Mfano ingine ni kanisa la Korintho. Mambo mingi sana iliingia kanisa la Korintho. Kitu kubwa walianza kufanya ni kunena kwa lugha au speak in tongues. Kama siku zetu na unaingia mahali na unafikiri mtu ameruka akili au ako na pepo. Paulo aliwaambia hawa sababu ya kuenena lugha na si mtu kusimama kama mjinga na kubabble na hakuna mtu anayejua anachosema. Paulo aliweka utaratibu wa kudhibiti uongo. Angalia Waraka wa kwanza wakorintho 14:27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. Nitakuuliza, umesoma hii mstari saa hii, wakati unaingia makanisa ambayo wananena lugha, wanafanya kama Paulo alituambia hapa kwa wakristo wakato tuko pamoja, kanisani? Wanene wawili au watatu? Na mtu anatafsiri kwao? Kwa nini? Kwa sababu si ukweli na uzoefu imeingia na wanafanya hivyo ili kupata majibu ya kihisia kutoka watu. Tena Mungu kwa neno lake alituambia ikiwa hii inafanyika ni naam na hiyo. Paulo anaendelea kwa vs.28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu. Unaona watu kufanya hii? Siku zetu watu hawaongeo lugha ambaye inaweza kutafsiriwa, nani atatafsiri kwao? Tena kwa sababu ni uongo na si kwa neno la Mungu. Wale watu watasema nini siku ile wanasimama mbele ya Mungu? Sisemi hii kwa sababu mimi ni mzungu au kwa sababu mimi ninaamini tofauti. Wale wanasema hawa ni wakristo na sisi nafikiri tunasoma bibilia moja, ukisoma kwa lugha yo yote inasema kama tumesoma saa hii. Tena niseme hapa, ikiwa wewe ni Mshariki ya kanisa lingine, ni mzuri kuuliza pastor au viongozi wako, sababu unafanya ibada yako kama unafanya, usikubali kusikia kwa sababu bibilia inasema, nionyeshe, wapi, kitabu gani, mlango gani, mstari gani. Mara mingi nimeuliza mapastor wingi, kwa nini wanafanya jinsi wanavyofanya, karibu wote walijibu kwa sababu walipata naam na hiyo, au kwa sababu hawajui njia ingine. Bibilia iko wapi? Tunakutana kuabudu Mungu wetu, Mungu wa Bibilia, anatuambia kama anataka kuabudiwa, si ngumu, lakini pia haitaleta pesa mingi kwa sadaka, haitaleta watu wengi kwa kanisa lako, haitaleta umaarufu. Kwa sababu wakati unafanya kama Mungu anasema, ni kumhusu yeye, si wewe.
Sasa nataka sisi kuona vitu ambavyo wakati tunakuwa pamoja kama watu wa Mungu, kanisa, Mungu anasema tufanye. Si kama tumewachwa bila kujua. Kumbuka mstari yetu ya leo Waraka wa kwanza watimotheo 3:15 upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Sisi tunataka kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu. Lazima sisi sote tujipime na tuangalia moyoni mwetu na kuuliza ikiwa tuko tayari kufanya na kubadilika ikiwa tunasoma kwa neno. Ni mzuri tunakumbuka Kumbukumbu la Toarati 5:32 Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na Bwana, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kuume wala wa kushoto.
Wakati yesu aliongea na ule mama wa samaria kwa kisima. Alisema kitu cha ajabu sana, kitu ambacho ilibadilisha jinsi watu wanavyoabudu mungu. Angalia Yohana 4:21-24 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Haya maneno ya Yesu yalishangaza wayahudi na wale ambao walimwabudu Mungu kwa miaka elfu mingi. Kwa nini? Kwa sababu Yesu alionyesha njia ya kweli watu wake watamabudu, na si kama walifikiri. Kwa hizi mistari Yesu anasema hii neno kuabudu mara nane. Ni ajabu sana. Yesu anasema hapa Kwa vs.23 Baba Mungu anatafuta watu ambao watamwabudu katika Roho na kweli.
Kitu cha kwanza ni kwa Roho. Hii inamaanisha nini? Sisi hatuwezi kumwabudu Mungu bila kuwa na moyo safi. Sisi tunaweza kufika hapa kila jumapili, tunaweza kuketi, kuimba, kuomba na kufanya kila kitu tunafanya hapa kwa ibada yetu na ikiwa moyo wako iko na unafiki ndani yake, Mungu hawezi kupokea hii ibada. Angalia maneno ya Yesu kwa Mafarisayo Mathayo 15:7-8 Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Uliona? Yesu anasema huniheshimu kwa midomo yenu. Wengi leo asabuhi wamekuwa pamoja kuabudu Mungu wao na walitumia mdomo wao, labda walifundisha, walihubiri, walisoma neno, waliomba, labda walisimama hapa mbele na waliimba, wewe kuketi hapa leo na uliimba, ulitumia mdomo wako, kuangalia ni kama umemheshimu Mungu kumwabudu, lakini yesu anasema lakini moyo yao iko mbali nami. Hii ni shida ya sisi binadamu. Tunaweza kuingia utaratibu fulani, hata bila kufikiria jinsi tunavyofanya. Mdomo unatembea lakini moyo wako iko mahali ingine. Na anagalia kama yesu anasema kuhusu watu ambao wanamwabudu naam na hiyo. vs.9 Nao waniabudu bure. Ni bure, ikiwa hii ni wewe au mimi na tulifika hapa leo asabuhi kama hii, ni bure. Kuenda kanisa imekuwa kawadia sana, nani alifikiria leo asabuhi jana jioni? Nani alijitayarisha moyo wake jana usiku, nani aliomba kuhusu ibada yetu ya leo, janan usiku, nani waliongea kuhusu watoto wao jana usiku kuwatayrisha kuingia kanisa leo asabuhi? Lazima sisi sote tuchunge sana. Tunaweza kuingia kwa sababu ni kawaida na ibada yetu inaweza kuwa bure. Kuabudu Mungu kwa Roho ni lazima tunaingia kwa mawazo na mioyo yetu na yakuwe safi, ikiwa ulipata uko na dhambi maishani yako na wewe ni Mkristo, usiingie kuwmabudu Mungu bila kutubu kwanza. Jitayarishe mapema kuingia kuabudu Mungu wako.
Nataka ninyi kujua na kusikia kanisa ya siku zetu na kama watu wanasema wanamwabudu Mungu ni hatari sana. Hii si mchezo. Hata Daudi alielewa umuhimu wa jinsi tunavyofanya ibada yetu. Aliandika kwa kitabu cha Zaburi 24:3 Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Leo asabuhi sisi tunasema tumeingia mbele ya Bwana wetu kumwabudu. Wakati uliingia leo asabuhi ulikuwa na hofu yo yote? Hakuna mtu aliogopa, kwa sababu tumesahau umuhimu ya hii, kusema ukweli tumefundishwa kwa miaka mingi vibaya, sisi tunakuja mbele za Mungu aliye hai, muumba wa vitu vyote bila woga wowote. Nani anaweza kuingia ukweli mbele ya Mungu wetu? Angalia Zaburi 24:4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.
Kitu cha pili yesu alisema kwa ule mama wa Samaria ni Kumwabudu Mungu na kweli. na ni muhimu kuona, kweli inaenda pamoja na Roho. Huwezi kumwabudu Mungu kwa kweli bila Roho na huwezi kumwabudu Mungu kwa Roo bila kweli. Tunapata ukweli wapi? Kwa neno la Mungu. Kama tumesema Mungu wetu ametuambia jinsi anastahili kuabudiwa. Wakati sisi tunakuja pamoja anasema kufanya vitu;
Kitu cha kwanza ni maombi. Wakati sisi tunakuja pamoja kumwabudu Mungu wetu, laizma tuongee na yeye. Jaribu kufikiria watu kuingia nyumba ya mtu na hata hawaongei na yeye. Naam na gani? Ni wengi wanaongea kumhusu Mungu lakini hawaongei na yeye. Lazima sisi pamoja kama watu wake wakati tunakuwa pamoja tunaomba. Hii ingekuwa sehemu kubwa ya ibada yetu. Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nataka sisi hapa kuwa kanisa ambalo tunaomba wakati tunakuja pamoja kuabudu Mungu wetu.
Kitu cha pili wakati sisi tunakuja pamoja Mungu anasema kufanya ni Kusoma Bibilia. Hii ni muhimu sana. Tunafungua neno la Mungu wetu na tunasoma. Paulo alimwambia Timotheo Kwa Waraka wa kwanza watimotheo 4:13 Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma. Ukisoma kwa kiingereza itasema Mpaka nitakapokuja, zingatia usomaji wa Maandiko hadharani. Kitabu hiki tunabeba nasi ingekuwa kama hazina kwetu, kwa sababu ni neno la Mungu wetu. Kila kitu kitu kuhusu Mungu wetu, Mwokozi wetu, maisha haya na maisha ambaye inakuja imeandikwa hapa, tungependa sana kueketi pamoja na kusikia wakati mtu anasoma.
Kitu cha tatu Mungu anasema kufanya kwa ibada yetu ni kuhubiri neno. Ni kufundisha watu wa Mungu neno lake. Ukiangalia hii mstari ya mwisho tulisoma kuhusu kuomba, utaona Paulo kuendelea kusema Mpaka nitakapokuja, fanya bidii katika kusoma Maandiko mbele ya watu wote, kuonya na kufundisha. Pia tunasoma kwa Waraka wa pili watimotheo 4:2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Tena nataka kusema hapa, kuhubiri neno si kusimama mbele ya watu na kutoa jasho na mate na kupiga kilele mingi na kukimbia juu ya viti na kurudia tena na tena, maneno yako. Mahubiri wingi ya siku zetu ni kama wako na mapepo ndanu yao, si Roho ya Mungu na ni kama watu walijiunga na Madhehebu fulani, Cult, si kanisa la Mungu. Hatutaki kusikia ujinga wa mtu fulani kusimama mbele yetu na kutuambia hekima ya dunia hii, tunataka kujua Neno la Mungu wetu linasema nini.
Kitu cha nne Mungu anasema kufanya ni Kuimba neno lake. Si kusimama mbele ya watu na kucheza na shingo yako. Pole, lakini ni ukweli. Kuimba neno la Mungu ni kutumia maneno, si maneno yo yote lakini maneno ya Mungu. Tenzi zetu zinajaribu sana kuinua neno la Mungu na mafundisho ya neno la Mungu. Angalia Waefeso 5:19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; Pia ninapenda sana Wakolosai 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Anasema nini ? Bila kujua neno ni ngumu sana kuonyana kwa zaburi, na nyimbi na tenzi za rohoni. Hii yote ingetoka kwa neno la Mungu wetu si kwa desturi letu, si kwa hii dunia.
Kitu cha tano Mungu anasema kufanya ni Sakramenti mbili ambazo ni ubatizo ya meza ya Bwana. Vitu hivi mbili Yesu Mwenyewe alisema kufanya na mdomo wake. Tunaona kwa kitabu cha Mathayo 28:19 enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; Kwa sababu ya kuhubiri neno la Mungu watu wanasikia na Mungu anatumia neno lake kubadilisha watu. Imani inakuja kwa kusikia neno la Kristo. Baada ya hii wanakuwa Wanafunzi wa Yesu na Yesu alisema wakati hii inafanyika kubatiza hawa. Ubatizo ni ishara ya kwamba wewe ni wa Yesu, na unataka wote kuona na kujua hii. Hii ni sehemu kubwa ya ibada yetu. Pia meza ya Bwana. Wakati sisi tuko pamoja ni mzuri tunakumbuka yote Yesu alifanya kwetu. Tena siku ya mwisho Yesu alikuwa pamoja na wanafunzi wake tunasoma kwa Waraka wa kwanza wakorintho 11:23-26 mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Unaona, Yesu alisema Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Sisi watu wake wakati tunakuwa pamoja na tunafanya hii tunaitangaza mauti ya Yesu hata ajapo. Ni muhimu sana.
Si kama vitu vingine ni mbaya au ni dhambi lakini tukikaa ndani ya vitu hivi vitano kwa ibada yetu, tutampendeza Mungu wetu, kwasababu ni vitu amabvyo yeye mwenyewe alisema kufanya.
Ni mzuri sisi sote tufikiria kanisa letu hapa kwa AIC Sekenani na ikiwa tunafanya vitu ambavyo Mungu haisemi kufanya ni vyema tubadilika. Nataka sisi sote kuwa na moyo wa Kumpendeza Mungu wetu. Ikiwa wewe unaenda kanisa lingine na wanafanya vitu ambavyo si mzuri, ni nje ya neno la Mungu, uliza viongozi kueleza zaidi na kukuonyesha kwa neno sababu wanafanya vitu vile. Ikiwa wewe si mshariki wa kanisa fulani, tafadhali ni mzuri unashika uko nje ya mpango ya Mungu kwa watu wake, alitaka sisi sote kuwa sehemu ya local church, si kuenda tu, lakini kuwa sehemu ya ile mwili. Mungu akipenda tutaongea kuhusu hii wiki ijayo. Ikiwa hujui Yesu, uko nje ya hii yote na ni njia moja tu kuingia na hii ni kuweka imani yako katika Yesu kristo, kutubu, kuamini na kutii neno lake. Ukitaka kufanya hii tuko hapa kuongea, unaweza kukaa kwa kitu chako na baada ya iabda yetu wakati watu wametoka tutakuja kwako.
Asanteni sana, Bwana wetu Yesu kristo Aifiwe na karibuni wiki ijayo.
Related Media
See more
Related Sermons
See more
Earn an accredited degree from Redemption Seminary with Logos.