Worship Pt.2 No longer on this mountain John 4:21
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 6 viewsNotes
Transcript
Leo asabuhi tunaendelea na masomo yetu kwa kitabu cha Yohana na tumefika Yohana 4:21. Kufika hapa tumeona mambo mingi sana lakini kwa mlango wa nne tumeona Yesu anaongea na Mwanamke Msamaria na walianza kongea kuhusu ibada ya Mungu. Tuliona wiki ikiopita Wakati ibada yetu ni mbaya ni shida kubwa sana kwa sababu lazima tufanye ibada yetu kulingana na neno la Mungu. Si kama tunahisi au kama sisi tunataka kufaya lakini lazima tunabudu Mungu jinasi anavyotaka kuabudiwa. Leo tunaona Yesu kusema ibada sio tena kuhusu mahali. Kumbuka huyu Mwanmke aliuuliza yesu mahali ya kuabudu Mungu ni wapi kwa sababu kwa Wasamaria walifanya hii kwa mlima inaitwa Gerizim na Wayahudi walisema ni Yerusalemu kwa sababu kwa agano la kale Mungu alichagua Yerusalemu. Leo yesu atasema kitu cha ajabu na hata leo Wayahudi kwa Israeli hawawezi kukubali. Bado wanaona Yerusalemu ni mahali pa kuabudu Mungu wao.
Mambo ya ibada kusema ukweli ni kati kati ya sababu yetu ya mwanadamu. Kila mtu, niseme tena, Kila mtu anabudu kitu. Tuliumbwa naam na hiyo. Maandiko inatuambia tuliumbwa kwa Mungu Angalia Warumi 11:36 vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Lakini kwa sababu ya dhambi, ibada imechafuliwa. Mara mingi watu wanabudu vitu kuliko Mungu. Mtume Paulo alieleza vizuri sana kwa Warumi 1:25 waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Tunaona hii ukweli kila siku. Uko na watu wanabudu pesa, wengine faraja ya maisha, wengine ufaulu, wengine hata wanabudu dini yenyewe. Swali si ikiwa tuabudu lakini tunabudu Mungu ipasavyo. Leo kwa mstari yetu Yesu anatuonyesha ya kwamba ibada ya kweli si kuhusu mahali tunaenda lakini jinsi tunavyomjia Mungu na kupitia nani tunamjia.
Tusome mstari yetu ya leo kwa muktadha yake Yohana 4:20-24 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Hii ni neno la Mungu wetu.
Tuombe:
Baada ya huyu7 Mwanamke kuuliza mahali gani kuabudu Mungu Yesu anasema vs.21 Mama, unisadiki. Sijui kwa nini kiswahili ilitafsiriwa tena hapa, Mama, tena si mzuri, ikiwa uko na bibilia ya kiingereza utaona inasema Mwanamke, niamini, Tena ni kama kusema Madam. Haijakuwa mbaya hata ilikuwa kuonyesha heshima kama tuliona kwa 2:4 wakati aliita mama yake Mariamu Mwanamke. Lakini ni mzuro tunaona kama yesu anaongea na huyu Mwanamke. Hasemi, nafikiri, according to me, au labda, anasema nini> Niamini. hii ni lugha ya mtu ambye ako na mamlaka. Yesu hapa si sauti ya mwalimu na anatoa mawazo yake au mapendekezo yake, Yesu ni mwana wa Mungu na wakati anaongea ni ukweli.
Ni mzuri kwetu wakristi kushika umuhimu wa neno la Bwana wetu. kwa maandiko Mungu anaita watu wake kuamini neno lake. Imani yetu hata ni kuamini jinsi Mungu yetu anavyosema. Hapa Yesu anazungmuza kwa hii njia. Anaweka maneno yake kuwa sawa na Mungu. Wakati yesu anafundisha hasemi kwa mamlaka ingine, yeye mwenyewe ni mamlaka. Tunasoma kwa Mathayo 7:29 akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao. Tunasoma mara mingi Yesu kusema kweli kweli niseme kwako. Hii ukweli ni yeye peke yake ako nai. Wakati tunasoma Yesu kusema “Niamini” anasema kuwa na imani katika mimi. Ni mzuri sisi oste tunajua kitu, kuamini Yesu Kristi ni kuamini mungu. Kumkataa Yesu ni kumkataa Mungu. Yohana anasema kwa Yohana 5:23 watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka. Hii yote ni muhimu kufahamu kwa sababu kama yesu atasema kwa huyu Mwanamke itaharibu miaka mingi sana ya ulewa wa kidini. Yesu ako karibu kusema tumefika mwisho wa ibada inayotegemea mahali, akokaribu kumwambia huyu Mwanamke na sisi sote Mfumo wa agano la kale imeisha na kufika kwa njia mpya ya kumkaribia Mungu imefika. Ikiwa Yesu ni mwalimu fulani hawezi kusea vitu hivi, ikiwa yesu ni nabii fulani hawezi kusema hii lakini Kristo anaweza kwa sababu yeye ni Bwana. Kabla ya unasikia kama Yesu anasema ni lazima tunajua yeye ni nani. Yeye ndiye Kristo, maneno yake yako na mamlaka. Bado leo asabuhi wakati tunasoma bibilia ni mzuri kujau hii ni neno la Kristo na hata leo iko na mamlaka. Wakati inasema kutubu na kuamini, ni lazima. wakati inasema kupenda jirani yako kama nafasi yako, ni lazima. wakati inasema kupenda bibi yako kama nafsi yako na mke ajitiishe kwa mumewe na watoto watiini wazazi wao, ni lazima. wakati inasema kuniabudu naam na hiyo ni lazima. Kile Kristo anachosema, lazima kiaminiwe, lazima kitiiwe. yeye ni Mungu. Usisemi unampenda Mungu na hufanyi kama anasema.
Yesu anaendelea kuongea na huyu Mwanamke na baada ya kusema niamini anasema saa inakuja. Tunaona hii mara mingi kwa injili ya Yohana. Sasa hii si kumaanisha kama saa fulani kwa saa yako lakini inamaanisha kwa historia ni kitu kubwa inafanyika. Ni mpango ya Mungu kuokoa watu imefika. Tunaona kwa kitabu cha Yohana hii inamaanisha Kifo cha Yesu, Ufufuo wa yesu na Wakati yesu anapoinuliwa. wakati Yesu anasema hii saa inakuja, ni kusema atakamilisha ukombozi kuptita msalaba na hii itabadilisha kila kitu hata njia tunaabudu mungu. Ni kusema ni agano ingine inaingia. Kama Mungu anafanya na watu wake itakuwa tofauti kabisa. Ni siku ile Yeremia alitabiri kuhusu kwa Kitabu cha Yeremia 31:31 siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya. Hii ahadi inatimizwa kayika Yesu Kristo. Kwa kifo na ufufuo wa yesu, alileta agani jipya katika damu yake. Ni mzuri sisi tunashika kitu cha umuhimu sana Sisi leo panda hii ya msalaba ni rahisi kwetu kuhukumu wale wengine. Lakini Kwa miaka ulfu moja wayahudi waliabudu Mungu kwa hekalu na walikuwa na mfumo wao kufanya hii yote. Sasa Yesu anaingia na anabadlisha kila kitu. Hii mfumo yao kati kati yake ilikuwa hekalu, na dhabihu na makuhani pekee walifanya hii. Na sasa yesu anasimama hapa kusema hii yote iko karibu kubadilishwa. Tunasoma kwa Wahebrania 10:9 Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili. Hii inaongea kuhusu Yesu. Hii si kusema agano la kale haina maana lakini ni kusema imetimizwa ndani ya yesu. Wakati yesu anasema saa inakuja, anatangaza utimilifu wa mpango wa Mungu, anasema agano jipya imefika, kila kitu iko karibu kubadilika na njia watu wanabudu Mungu haitakuwa kama ilikuwa.
Si bure watu wingi kama Mafarisayo na viongozi wa wayahudi hawajapenda yesu. Unajua Hekalu kwa miaka elfu moja ilikuwa mahali utafika mbele ya Mungu. Nje ya hekalu huwezi. Mahali ni Mungu amesema, nyumba ilikuw akama Mungu alisema, Makuhani kama Mungu alisema na mfumo ya dhabihu kama Mungu alisema. Hii yote ilikuwa lazima kufika mbele ya Mungu ambaye mtakatifu. Watu kama sisi ikiwa tulitaka kuingia mbele ya Mungu lazima ni kufanya kama Mungu alisema. Kusema ukweli watu kama sisi, Mataifa hatuwezi. Na siku zile huwezi kuabudu Mungu mahali yo yote wakati wo wote, lazima ufike Yerusalemu. Nafikiri sisi hatushiki uzito wa kuabudu Mungu na uhuru tuko nai katika Yesu kristo. Ni zawadi kubwa sana kuishi kwa wakati wetu. Hii yote ya miaka elfu moja kuabudu Mungu ilikuwa kuweka macho ya watu kwa kitu ambacho inakuja, kitu ambacho mi mzuri zaidi. Saa inakuja, Kitu kipya iko karibu kufanyika, na hii yote itakuwa tofauti.
Angalia kama yesu anaendelea kusema kwa Yohana 4:21 saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Kwa mtu yo yote kusikia hii, bila shaka huyu Mwanamke wa Samaria kusikia hii alishangaa. Kwa myahudi kusikia hii ingekuwa ajabu zaidi. Yesu anasema iko karibu hamtamwabudu baba katika mlima huu, au hata Yerusalemu. Hii ni kusema jambo la kuabudu Mungu kwa mahali fulani iko karibu kuisha. Kama siku zetu ni kama watu wanafikiri unabudu Mungu jumapili kwa mahali inaitwa kanisa. Mawazi kama hii ni sababu watu wanaishi maisha yao kwa chafu jumatatu hadi jumamozi. Siku hizi watu wanafikiri tunaishi kwa agano la kale na ni siku moja ya wiki watu wa Mungu wanakuja kwa mahali fulani kuabudu yeye. Sisi tunaweza na tungeabudu Mungu wetu kila siku, tuko na hii uwezo kwa sababu ya yesu kristo. Mfumo yao ya wayahudi, hekalu, dhabihu, ukuhani, yote ilikuwa kuweka macho yao mbele, na sasa mbeoe imefika na anasimama kuongea na huyu Mwanamke. Njia mpya ya kumkaribia Mungu ilikuwa hapa. Yesu kufika ilifungua mlango kwa watu wote kwa dunia nzima kuabudu Mungu.
Sasa yesu kusema hii, lazima unajua shida inakuja. Kwa historia nzima, tangu mwanzo wa dunia, maneno ya Yesu hapa yanabadilsha mambo mingi. Yerusalemu ilikuwa kila kitu. Hekalu ya Mungu ilikuwa, Mungu alikuwa hapo. Bila Yerusalemu kwa wayahudi walipoteza njia ya kufika mungu wao. Hata Daudi alisema kwa Zaburi 27:4 Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake. Hekalu ilikuwa mahali mbinguni na dunia walikuja pamoja. Sasa hapa Yesu anasema hii yote inaenda. Kwa nini? Angalia Wahebrania 10:1 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, Hii mfumo ilikuwa na sababu na sababu yake ilikuwa kuweka macho ya wote mbele kwa kitu kiingine, Yesu, na amefika. Hata wakristo leo ambao wanaishi kwa agano la kale ni mzuri kujua, Mtu mwengine amefika na ametimiza hii yote na anaitwa yesu. Weka tumaini na imani yako kwake, si kwa mfumo fulani.
Nataka ninyi kujua ya kwamba sisi hapa tunaamini. Agano la kale si tofauti ya agano jipya. Agano la kale ilitimizwa katika Yesu. Agano la kale ilikuwa muhimu sana na story yake ilikuwa ahadi amabye itakuja, agano jipya hii ahadi ilifika. Agano la kale imejaa na kama tumesoma kwa wahebrania 10 kivuli. Kivuli ni kitu ambacho inatuonyesha kitu ambacho inakuja. Tuko na mifano mingi ya kivuli. Moja ni hekalu. Hekalu ilikuwa kivuli cha Mungu kukaa na watu wake. Inweka macho yetu mbele wakati Yesu Kristo atakuja na atakaa na watu wake, wakati wo wote si kwa mahali. Kwa agano la kale tuliona dhabihu, walifanya hii kila mwaka kwa sababu hawawezi kutoa dhambi kabisa, waliweka maccho yetu kwa yesu na dhabihu yake ilikuwa mara moja na iko na uwezo kutoa dhambi zako kabisa mbele ya Mungu. Ukuhani kwa agano la kale ilikuwa kivuli ya watu kusimama kati kati ya watu na Mungu. lakini hawa walikuwa wenye dhambi, Yesu alikuwa mkuhani kamilifu na sasa ni yeye anasimama kati kati ya sisi na Mungu. Sasa kwa sababu Yesu amekuja hakuna hitaji ya kivuli tea, hakuna hitaji ya mifano ya kuweka macho yetu mbele, mbele amefika, sisi hatuishi kwa kivuli tunaishi katika uhalisia.
Yesu ni hekalu ya ukweli. Hii ni mahali kila kitu inakuja pamoja. Kumbuka wakati Yesu alisema kwa Yohana 2:19 Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha. Watu ambao walisikia hii hawajafahamu maana yake. Walifikiri Yesu anaongea kuhusu hekalu ya mawe na Yohana anasema kwa 2:21 alinena habari za hekalu la mwili wake. Yesu mwenyewe ni hekalu la kweli. Ibada yote inapitia kwake. Kumbuka hekalu kwa gano la kale ilikuwa mahali wa uwepo wa Mungu. Ilikuwa mahali ya dhabihu, mahali wenye shambi walikuja kukutana na Mungu. Na sasa hii yote iko ndani ya Yesu. Uwepo wa Mungu si kwa nyumba ya mawe, iko ndani ya yesu, dhabihi hakuna hitaji kwao kwa sababu Yesu alilipa dhabihu na ilikuwa kamili. Angalia wahebrania 10:12 alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, Dhabihu ya Yesu ni ya milele, hakuna kurudi kila mwaka. Wenye dhambisi lazima wanakuja kwa mhali fulani kukutaa na Mungu, wanakuja kwa mtu, tunasoma kwa Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Kwa kifo cha Yesu kitu cha ajabu kilifanyika. Angalia Mathayo 27:51
