Tamaa ya kua mbele zake Bwana
Sermon • Submitted • Presented
0 ratings
· 83 viewsFiles
Notes
Transcript
Zaburi 84:8-12
1. Jinsi gani yanavyopendeza makao yako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi!
2. Nafsi yangu yatamani mno maskani ya Mwenyezi-Mungu! Moyo na mwili wangu wote wamshangilia Munga aliye hai.
8. Usikie sala yangu ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi; unitegee sikio, ee Mungu wa Yakobo.
9. Ee Mungu, umwangalie kwa wema ngao yetu mfalme, umtazame huyo uliyemweka wakfu kwa mafuta.
10. Siku moja tu katika maskani yako, ni bora kuliko siku elfu mahali pengine; afadhali kusimama mlangoni pa nyumba yako, kuliko kuishi nyumbani kwa watu waovu.
11. Mwenyezi-Mungu ni jua letu na ngao yetu; yeye hutuneemesha na kutujalia fahari. Hawanyimi chochote kilicho chema, wale waishio kwa unyofu.
12. Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, heri mtu yule anayekutumainia wewe!
Zaburi 84:1,2,8-12
v.8&9 Unakitamani kile unachokijua na kina faida kwako, muandishi wa Zaburi anatuonyesha. Ni BWANA; jina la Mungu wa kweli kwa mtazamo yakua yu hai na anauhusiano na watu wake, watu wa agano. Hii ni kweli kwako wewe ambaye uko ndani yake kristo yakwamba huyu Mungu ambaye yu hai na niwa agano ni Mungu wako kupitia kwake Yesu Kristo
Na pia ni Mungu wa majeshi, kumbuka waisraeli walikua watumwa Misri, Munu akawapigania, ingawa hawakukua na jeshi, walikua na silaha Muhimu zaidi. Walikua na Mungu wa Mejshi. Akawapigania dhidi ya Farao, na kuwapa ushindi wiki baada ya wiki kama kanisa kunayo nafasi ya kushuhudia kile ambacho Mungu amekutendea. Mara kwa mara ninapowaskia, wanasema ama tunasema, Mungu amenitendea. (Nashuhudia naona Yesu ananipenda) kwa kusema kwa namna nyingine ni yakwamba Mungu wa majeshi amekupigania vita ambazo kwa uwezo wako haungefaulu.
v.10 Siku moja tu katika maskani yako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine.
Krismasi (Noel) si siku muhumu kwa wengi. Nyumbani ilikua hio ndio siku ya chapati, mchele, labda soda a kupiga picha kwa sababu ya nguo mpya. Labda yako ni siku ya kuzaliwa, ama siku ya graduation ama harusi yako. Krismasi kwangu hata kabla ya kua Mkristo ilikua muhimi, na ningeutarajia kwa sababu 1. Likizo ya shule, 2. Chakula na 3. Kupiga picha.
Mwandishi wa Zaburi angutuhimiza ya kwamba Krismasi kwake ni kua katika maskani pake Mungu. Kunasherehe ambayo ni uzima wa milele. Paulo katika Warumi 6:23 anatuhimiza hivi; kwa maana mshahara wa dhambi ni kifo/mauti, lakini zawadi anayotoa Mungu ni uzima wa milele katika kuungana na Kristo Yesu Bwana wetu. Hii ni zawadi bora kuliko zawadi yeyote utakayo wahi kupata. Yesu mwanawe Mungu anazidi zawadi ya gari, anazidi zawadi ya fedha, anazidi miujiza ya uponyaji wa huu mwili ambao unazeeka na utakufa. Kwa sababu Mungu amekua zawadi yako. Heri siku moja mbele zako, Krismas yangu ni kua pamoja na wewe. Siku moja mbele zako ni bora kuliko makrismas elfu za picha na chakula. Naweza nikapenda na kufurahia siku kwa sababu ya vitu. Kama siku ya kuzaliwa ama Krismasi, naweza nikazingojea hizo siku kwa sababu ya zawadi nitakazo pata.
Lakini ni bora kufurahia siku kwa sababu ya mtu, vitu havikukufia msalabani. Mtu alikufia msalabani!!! Yohana katika Yohana 3:16 kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akakitoa kitu chake cha pekee??? Hapana alimtoa *mwana wake wa pekee. Ili yeyote amuaminiye aspotee bali awe na uzima wa milele. Heri siku moja mbele zake (Yesu) Kristo kuliko siku elfu mbali na yeye.
Afadhali kuwa bawabu mlangoni mwa Mungu, kuliko kuishi katika hema za uovu.
v.11 Bwana Mungu ni jua na ngao; Mungu ndiye chanzo cha mwangaza kwa wale wanao mtamarii (Zaburi 119:105). Neno lako ni toa kwa miguu yangu na mwanga, kwa njia zangu. Na pia ni ngao kwa wale wanaomtegemea. Ngao inakukinga kutokana na maovu yanaomushwa dhidi yako.
Bwana hatawanyima kitu chema, hao waendao kwa ukamilifu. Mtu mkamilifu ni mtu wa aina gani?? Huyu ni mtu ambaye amekamilika kwa sababu ya kazi ambayo Kristo alitenda msalabani. Si wa kukuja kanisa, si kwa kufunga. Si kwa kutoa zaka, si kwa kusaidia maskini amechochote tunachotenda ndio tunakamilika. Tu wakamilifu kwa sababu ya kazi aliyotenda Kristo. Yohana 19:30 Yesu alisema imekwisha!
Bwana hatawanyima kitu chema wale waishio kwa ukamilifu. Ee Bwana wa majeshi heri mwanadamu anayekutu mainia wewe.
Je, unamtumainia Bwana wa majeshi? Tumaini lako liko kwa nini ama nani? Je unamtamani Bwana wa majeshi, Mungu wa agano na watu wake, Mungu wa kweli?
Mwaka umeanza, kuna shughuli nyingi za hapa na pale, mahitaji moja baada ya nyingine, unamalengo kadhaa ungependa kutimiza, labda nina shule, labda ni kazi, labda ni kijamii unataka uwe mahali fulani kabla mwisho wa mwaka.
Je, mojawapo ya malengo yako ni kumtamani Mungu na kwa mbele zake?
Huwezi ukamtamani mtu ambaye humjui kama humjui, ni fursa nzuri kuwa na uhusiano na huyu Mungu wa kweli. Yuko hapa, ni kwa sababu yake ndio tume kutana leo kunaye ambaye hamjui huyu Mungu na angependa kumpatia maisha yake leo? Usisite, usiogope, huenda huu ndio fursa ya Mwisho anakuia kwake kama utakubali. Je tunaye?
Tamaa ya kua mblele za Bwana
1.Unatamani mtu unaye mjua
-Bwana
-Mungu wa majeshi
2.Tamaa ulio nayo kwake Mungu lazima iwe kubwa ama zaidi kuliko tamaa uliyo nayo ya vitu vingine.
-Krismasi
-Mtu alinifia msalabani, si vitu (Yohana 3:16)
-Heri siku moja mbele zako Kristo
-Afadhali kua bawabu mlangoni mwa bwana
3.Mungu ni Jua na ni ngao hata mnyima kilicho chema, yeyote aliye mkamilifu
Zaburi 119:105. Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga kwa njia zangu
